Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akifutiliana kwa makini pambano la soko kati ya timu ya Black burn na Nondo. Kulia ni Katibu Msaidizi wa Chama cha Soko Wilaya ya Pangani, Mohamed Swazi, katika pambano hilo timu ya Black burn iliibuka na ushindi wa bao 4-1. (Picha zote na Mpiapicha wetu, Tanga)
Mbunge Amina Mwidau, akikagua timu huku akiwa na viongozi wa timu ya Blackburn kabla ya mchezo kuanza.
Mbunge Amina Mwidau, akikagua timu huku akiwa na viongozi wa timu ya Blackburn kabla ya mchezo kuanza.
Mgeni rasmi katika mashindano ya Mwidau CUP, Amina Mwidau akijadiliana na jambo na viongozi wa Chama cha Soka Wilaya ya Pangani, huku Nahoddha wa timu ya Nondo FC, Ahmad Juma akifuatilia na katikati ni mwamuzi wa pambano hilo, Mbaruk Suleyman Mohamed.
Mgeni rasmi Amina Mwidau, akizindua mashindano ya soka ya Mwidau CUP kwa kupiga mpira.
Mbunge Amina Mwidau akikabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya soka ya wanawake ya Sawaka Sport Club, Monica Frank Mbaruk.
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau kupitia Chama cha Wananchi(CUF), amezindua rasmi ligi ya Mwidau Cup inayoshirikisha timu 45 za Wilaya ya Pangani yenye kata 13 huku zaidi ya sh.milioni 20 zikitarajiwa kutumika hadi kumalika kwa ligi hiyo.
Kwa mujibu wa Mwidau lengo la mashindano hayo si kupata tu mshindi kwa ajili ya kuchukua zawadi, bali anataka kuona vipaji vya soka vinaibuliwa kwa kuwa soka ni ajira na wakati huo huohuwaunganisha wananchi pamoja na hiyo ndio dhamira yake kwa Wilaya ya Pangani na Tanga kwa ujumla.
Akizungumza katika Uwanja wa Kumba Wilayani Pangani wakati akizindua ligi hiyo, Mwidau alisisitiza umuhimu kwa timu ambazo zinashiriki kuonesha uwezo wao wa kusakata soka na anatamani kuona Wilaya ya Pangani inakuwa chachu katika maendeleo ya soka kwa mkoa wa Tanga.
“Malengo yangu ni kuona tunapata vipaji vya soka kwa vijana wetu maana uwezo wanao. Hivyo nimeamua kuanza na Wilaya ya Pangani kwa kudhamini ligi hii nikiwa na maana ya kupata sehemu ya kuanzia katika kuhakikisha Mkoa wa Tanga unakuwa na ligi ya aina hii,”alisema.
Alifafanua yeye ni mdau mkubwa kwenye michezo na amekuwa akitoa vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu na mpira wa wanawake lakini ni wakati muafaka wa kudhamini ligi na ndio maana ameamua kutoa sh.milioni 20 kuona michezo inapewa nafasi kwa kuwa na mashinano ya Mwidau CUP.
Akizungumzia zaidi kuhusu ligi ya Mwidau Cup, alisema kuwa ametoa vifaa ya michezo kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo na jumla ya thamani yake kuanzia vifaa na mambo mengine ya udhamini jumla ya sh.milioni 20 zitatumika lakini jambo la msingi kwake kuona michezo ndani ya mkoa huu inapewa kipaumbele.
Aliongeza kuwa yeye ni mbunge wa Mkoa wa Tanga , hivyo anayo fura ya kushirikiana na wadau wa michezo katika kuleta maendeleo na kuweka wazi historia inaonesha mkoa huo umekuwa maarufu katika michezo kutokana na wachezaji wengi maarufu kutoka mkoani hapa.
Hata hivyo alisisitiza nidhamu kwa vijana katika suala la michezo kwani, ndio njia pekee ya kufikia kwenye mafanikio na kwamba hata katika suala la maendeleo ili liweze kufanikiwa linahitaji nguvu ya wananchi kwa ujumla wao bila kujali itikadi za vyama vya siasa, hivyo mashindano hayo yatawaunganisha katika burudani lakini pia katika kufanya kazi kwa ushirikiano.
Mwidau , mbali ya kutoa vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu, pia alitumia nafasi hiyo kutoa vifaa vya michezo kwa timu ya mpira wa Netball kwa Wilaya ya Pangani huku akisisitiza kuwa amefanya hivyo kwenye maeneo mengine ya mkoa wa Tanga.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Wilaya ya Pangani, Mohamed Swazi, alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa chachu kwa vijana kutumia muda mwingi kujihusisha na michezo huku akitumia nafasi hiyo kufafanua changamoto iliyopo kwenye timu yao timu nyingi hazina vifaa vya michezo, lakini kwa uamuzi wa mbunge wa Mwidau wanaamini wamepata mwanzo nzuri wa kuendeleza michezo kwa kasi.
Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Pangani Kemmy Anatori, alisema kuwa anatambua umuhimu wa michezo na kwa upande wake akiwa mwakilishi wa Serikali anaunga mkono juhudi za Mwidau za kuhamasisha michezo kwenye wilaya yake kwani faida ni nyingi kuliko hasara.
Kwa timu ambazo zimefungua pazia ya ligi hiyo, timu ya soka ya BlackBurn imefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kuibamiza timu ya soka ya Nondo mabao 4-0.
No comments:
Post a Comment