Mwenyekiti wa Mtandao wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN), Mhandisi Margaret Munyagi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutanano kufunguliwa rasmi leo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mtandao wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN) leo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wajumbe wa Mkutano wa Mtandao wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN) leo, jijini Dar es Salaam.
Na Frank Shija - WHVUM
Wadau
wa sekta ya Utangazaji barani Afrika wametakiwa kulinda na kuthamini maudhui ya
ndani badala ya kukumbatia maudhui ya nchi za Magharibi.
Rai
hiyo, imetolea na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua mkutano wa Mtandao wa
Mamalaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika (ACRAN) leo jijini Dar es
Salaam.
Profesa
Elisante amesema ni faraja kubwa kuona kuwa wadau wa sekta ya udhibiti
mawasiliana wanashirikiana katika kutatua na kusimamia sekta hiyo muhimu kwa
pamoja kwa kuwa hiyo italeta nguvu na hari ya kusimamia maadili ya kiafrika kwa
sauti moja.
"Nafarijika
sana kuona mnavyo shirikiana katika kuhakikisha maudhui katika sekta ya
utangazaji hayaleti athari katika maadili yetu, hivyo ni seme tu Serikali
itazidi kushirikiana nanyi katika kusimamia hilo". Alisema Prof. Elisante.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Mamlaka za Mawasiliana Afrika (ACRAN)
Mhandishi Margaret Munyagi amesema kuwa pamoja na sekta hiyo kulazimika kuhamia
katika mfumo wa Dijiti bada Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano zinaendelea
kuhakikisha kuwa hakuna mwanya kwa mahudhi yanayokihuka maadili.
Mwenyekiti
huyo aliongeza kuwa kutoka na ushirikiano waliona wameweza kusimamia kwa karibu
misindi na maudhi ya utandazaji ili kulinda maadili ya Mwaafrika.
"Tokea
tuhamie mfumo wa Dijiti kumekuwa na ongezeko la masafa ya utangaziji lakini hili
halijaathiri udhibiti wa maudhui kwa kuwa tumejipanga kikamilifu na
tunashirikiana vizuri kuhakikisha maadili ya mwaafrika yanalindwa". Alisema
Mhandisi Munyagi.
Mkutano
huu wa Mtandao wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Afrika unafanyika ikiwa ni
mara ya pili Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu, ambapo miongoni mwa mambo
yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na namana Tanzania ilivyopiga
hatua katika kuhamia mfumo wa Dijiti. (Picha zote na Frank Shija - WHVUM)
No comments:
Post a Comment