Umoja wa Mataifa unasema kuwa visa vya ugonjwa wa kupooza au
Polio vimethibitishwa miongoni mwa watoto nchini Syria.
Wataalamu wanasema kuna hofu ya kuenea kwa ugonjwa huo katika kanda
nzima.Shirika la afya duniani WHO, linasema kuwa linasubiri matokeo ya uchunguzi wa maabara, waliofanyia watoto 12.
Shirika hilo pia linatathmini virusi vinavyosababisha ugonjwa huo ambavyo kuna uwezekano viliingia nchini humo kutokana na wapiganaji wa kigeni waliokuja kuwasaidia wapiganaji wa Syria.
Kabla ya mgogoro wa kisiasa kuanza Syria mwaka 2011, asilimia 95 ya watoto wa nchi hiyo walikuwa wamechanjwa dhidi ya ugonjwa huo.
Inakisiwa sasa kuwa watoto nusu milioni bado hawajapokea chanjo hiyo.
Katika nchi nyingi zinazostawi, ugonjwa wa Polio umeweza kudhibitiwa ingawa nchini Nigeria, Pakistan na Afghanistan ugonjwa huo ni janga kubwa.
Msemaji wa shirika la Afya duniani Oliver Rosenbauer alisema kuwa chanzo cha virusi inawezekana ni kutoka katika eneo lenye ugonjwa huo.
''Na hapo ndipo inawezekana ugonjwa hupo umetoka na ndio maana ni muhimu kuuangamiza ugonjwa katika maeneo hayo la sivyo ugonjwa huu utapatikana katika maeneo yasiyokuwa nao,'' alisema Oliver Rosenbauer
No comments:
Post a Comment