TANGAZO


Tuesday, October 29, 2013

Milioni wataka hatua dhidi ya wabakaji Kenya

 

Liz anataka hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wabakaji wake
Wanaharakati wanaopinga vitendo vya ubakaji wanapanga kufanya maandamano siku ya Alhamisi kulaani ukatili aliofanyiwa msichana mmoja wa shule nchini Kenya.
Hatua yao inakuja baada ya kisa cha msichana mmoja aliyebakwa na genge la watu sita kulemazwa wakati polisi hawakuchukua dhabu kali dhidi ya wabakaji hao.
 
Zaidi ya wakenya milioni moja wenye ghadhabu wametia saini ombi la kuishinikiza serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watu watatu waliotuhumiwa kumbaka msichana mmoja wa shule na kutupa mwili wake kwenye choo cha umma.

Ghadhabu yao inatokana na washukiwa kupewa adhabu ya kukata nyasi badala ya kuchukuliwa hatua za kisheria
Kitendo hicho kilizua hisia kali miongoni mwa umma kutokana na maafisa wa usalama kupuuza ukubwa wake.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 kwa jina Liz, alivamiwa na genge la watu sita waliomchapa na kisha kumbaka alipokuwa njiani kwenda nyumbani kutoka kwa mazishi ya babu yake magharibi mwa nchi.
Baada ya kitendo chao walimtupa chooni msichana huyo aliyekuwa anavuja damu na kupoteza fahamu .
Mnamo siku ya Jumatatu idadi ya waliotia saini ombi hilo kwa polisi kuchua hatua lililoanzishwa na mwanaharakati, Nebila Abdulmelik , ilipita watu milioni moja na idadi ya waliokerwa inaendelea kuongezeka.
"kuwaachilia huru wabakaji na kuwaadhibu kwa kukata nyasi , bila shaka hii ndio adhabu mbaya zaidi kuwahi kutolewa kwa kitendo kama hicho duniani, '' alisemaAbdulmelik. ''

Hili ni jambo baya sana na aibu kubwa kwa polisi kwa adhabu iliyochukuliwa dhidi ya watuhumiwa .
Msichana huyo aliwafahamu watatu kati ya wale waliomshambulia na walipelekwa kwa polisi na wanakijiji, kwa mujibu wa mamake msichana huyo.
"watatu hao waliamrishwa kukata nyasi katika bustani la okituo cha polisina kisha kuachiliwa. ''
Msichana huyo sasa anatumia kiti cha magurudumu mgongo wake ukiwa umeathiriwa vibaya kutokana na kuchapwa au kubururwa ardhini na pia alipata majeraha mabay sana kutokana na kitendo cha ubakaji.
''Ningependa kuona hatua ikichukuliwa dhidi ya walionitendea unyama huu,'' Liza aliambia gazeti la Daily Nation lililokuwa la kwanza kuripoti kisa hicho. ''Nataka wakamatwe na washitakiwe na kisha kaudhibiwa.
Wabunge pia wamekosoa vikali kitendo hicho.

No comments:

Post a Comment