TANGAZO


Tuesday, October 29, 2013

Miaka 35 jela kwa njama ya kumuua Mandela

 

Mike du Toit aliongoza kundi la kibaguzi la Boeremag kuwashambulia waafrika weusi na kupanga kumuua Mandela
 
Kiongozi wa njama ya waliokuwa wanaharakati wa kibaguzi nchini Afrika Kusini kumuua Nelson Mandela na kuwafukuza waafrika weusi kutoka nchini humo, amefungwa jela kwa miaka 35. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo.
 
Kiongozi huyo aliyekuwa mhadhiri wa huo kikuu Mike du Toit alipatikana na hatia mwaka jana kwa kosa la uhaini, kwa kukiokongoza kikundi hicho katika kupanga njama ya kumuua Mandela. Kesi yake ilisikilizwa kwa miaka 9.
 
Aliongoza kundi la wapiganaji wa Boeremag, wabaguzi wakuu wa kizungu nchini humo.

Mnamo mwaka 2002 wapiganaji hao walijaribu kuipindua serikali iliyokuwa inaongozwa na chama tawala cha ANC.

Wanachama wengine 20 wa Boeremag waliopatikana na hatia kwa kosa la uhaini, walihukumiwa jela kwa kati ya miaka mitano na 35 katika mahakama moja mjini Pretoria.

Mnamo mwezi Julai mwaka 2012 du Toit alipatikana na hatia ya mashambulizi ya mabomu katika mtaa wa mabanda wa Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.

Alikuwa mtu wa kwanza kuwahi kupatikana na hatia ya kosa la uhaini nchini Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994.

Wadadisi wanasema kuwa huku swala la ubaguzi likiendelea kuwa changamoto nchini Afrika Kusini makundi yenye itikadi kali za kibaguzi kama Boeremag, hayana ushawishi mkubwa.

No comments:

Post a Comment