TANGAZO


Friday, October 11, 2013

Vijana kutoka Mikoa mbalimbali washiriki mdahalo ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akizungumza na vijana kuhusu umuhimu wao katika ujenzi wa taifa wakati wa mdahalo wa Vijana katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA),``````````````````````` mkoani Iringa.Vijana hao wako katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013. (Picha zote na Aron Msigwa –MAELEZO)
Vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mdahalo wa Vijana leo mkoani Iringa.
Wananchi wa Mkoa wa Iringa wakipata taarifa mbalimbali kuhusu bidhaa na huduma zinazopatikana katika mabanda ya Maonyesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sparke International Co.Ltd Bw. Gerald Reuben akitoa elimu kwa baadhi ya Vijana waliotembelea banda la Maonyesho la  Kampuni hiyo katika viwanja vya maonyesho vya Mlandege mkoani Iringa.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la Maonyesho la Wizara ya Habari, vijana, Utamduni na Michezo mkoani kuhusu utendaji kazi wa Bodi hiyo na usimamizi wa kazi za wasanii nchini.


Wananchi wa mkoa wa Iringa wakipata taarifa  na kuangali picha mbalimbali za matukio ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa uhai wake katika banda la Maonyesho la Mfuko wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

No comments:

Post a Comment