TANGAZO


Friday, October 11, 2013

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete azindua mradi wa mafunzo ya Gesi na Mafuta ya Petroli VETA, mjini Lindi

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete  (wa pili kulia), akiwapungia mkono wanafuzi wa Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Lindi kabla ya kuzindua mradi wa mafunzo ya Gesi na mafuta ya Petroli jana mkoani Lindi. Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi na  wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro Hamidi.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (aliyevaa kitenge) akipata maelekezo kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), Edwin  Nduguru(kushoto) jinsi deep stick inavyofanya kazi ya kupima kiwango cha oil kilichopo katika injini ya gari alipotembelea karakana ya ufundi wa magari wa chuo hicho jana. Wanaoshuhudia tukio hilo ni  Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah  Moshi (kulia) , Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick   Mwananzila (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro  Hamidi (kushoto).
Mke  wa Rais Mama Salma Kikwete (aliyevaa kitenge), akiongea jambo  na  Meneja wa British Gesi Tanzania, ambao ndiyo wafadhili  wa mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli, Kate Sullam (kushoto) jana,  kwenye   Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), mjini Lindi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi.
Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete, akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana, kwenye Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), mjini Lindi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana, Chuo cha  Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi(VETA), mjini Lindi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila na wa kwanza kushoto ni Ofisa Uhusiano wa chuo hicho, Dora Tesha.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  (aliyevaa kitenge), akiwa  katika picha ya pamoja  na baadhi ya viongozi na wanafunzi  wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), mjini Lindi mara baada ya kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya petroli.
Mwanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Stadi (VETA), mjini Lindi akimwonesha Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (aliyevaa kitenge), kifaa cha kukata vyuma   katika karakana ya uungaji  vyuma.

Mwanafunzi wa  wa  Chuo cha  Mafunzo ya  Elimu ya 

Ufundi  Stadi (VETA), Lindi akimwonesha    Mke wa Rais 

Mama Salma Kikwete  (aliyevaa kitenge)  jana  kifaa cha  

ufundi wa magari katika karakana ya ufundi wa magari. 

(Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo)

No comments:

Post a Comment