TANGAZO


Friday, October 11, 2013

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), TCC wafadhili mafunzo maalum ya kuongeza uwezo wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi

Ofisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Masozi Nyirenda, akiwaelezea waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam leo juu ya ufadhili wa Mamlaka hiyo kwa  kushirikiana na Kampuni ya Sigara Tanzania (TTC) kwa mafunzo ya kuongeza uwezo wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi. Kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Misaada kwa Jamii toka kampuni ya Sigara Tanzania (TTC), Martha Saivoiye.
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe akielezea mipango ya Mamlaka hiyo ya kuendelea kutafuta wafadhili zaidi ili kuongeza idadi ya wanafunzi  kike wanaosoma masomo ya Sayansi. Katikati ni Ofisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Masozi Nyirenda na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Misaada kwa Jamii wa kampuni ya Sigara Tanzania (TTC), Martha Saivoiye.
Meneja Mawasiliano na Misaada kwa Jamii toka Kampuni ya Sigara Tanzania (TTC), Martha Saivoiye akielezea mikakati ya kampuni hiyo kuongeza ufadhili ili kuwa na idadi ya wanafunzi  wa kike wanaosoma masomo ya Sayansi. Katikati ni Ofisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Masozi Nyirenda na kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe  
Mratibu wa kozi ya awali toka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Mhadhiri Matara Ryoba akielezea namna ya kupata wanafunzi na uendeshaji wa kozi. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Frank Mvungi.
Mmoja wa wanafunzi waliomaliza kozi ya awali, Sai Charles akielezea furaha yake baada ya kumaliza kozi ya awali na kupata nafasi ya kuendelea  ngazi ya Stashahada ya Uhandisi wa Madini katika Taasisi ya Teknolojia, Dar es Salaam (DIT) cha jijini.
Baadhi ya Wanafunzi waliomaliza kozi ya awali katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), wakiwa katika hafla hiyo.


*VYUO  9 vyapatiwa ufadhili waTsh 879,816,788 kuendesha mafunzo ya kuongeza uwezo wawanafunzi wa kike kujiunga na masomo ya sayansi.

WANAFUNZI 1,861 wamenufaika namafunzo na kujiunga na masomo ya Diploma na shahada. 

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kuendelea kutoa ruzuku kwa taasisi za elimu kwa lengo la kuongeza ubora na nafasi katika upatikanaji wa elimu, pamoja na miradi mingine imelenga kupanua udahili wawasichana katika masomo ya sayansi katika vyuo vya ufundi na vyuo vikuu. 

Kumekuwa na utofauti katika idadi ya wanafunziwa kike na wa kiume wanaodahiliwa katika fani mbalimbali za sayansi katika Vyuo. Mamlaka ya Elimu Tanzania imetoa ufadhili kwa vyuo vinavyoendesha mpango maalum wakuongezea uwezo wanafunzi wa kike iliwaweze kujiunga na fani za sayansi.

TEA ilianza kufadhili mafunzo hayo ya Vyuo Vikuu mwaka 2005/2006 hadi 2012/13, ambapo shilingi za Tanzania million 879,816,788.00 zimetumika kutoa ufadhili huo.Wanafunzi waliofaidikani 1,861.   Taarifa za tathmini na ukaguzi za TEA pamoja na ripoti za taasisi husika zinaonesha wanafunzi wote walifaulu kuweza kujiunga na kozi mbalimbali.

Vyuo ambavyo vimefaidika na ufadhili huu ni Dar es salaam University College of Education (DUCE), College of Engineering and Technology (COET)-UDSM, State University of Zanzibar (SUZA), Dar es salaam Institute of Technology (DIT),  Arusha Technical College , Karume Institute  of Science &Technology,  University College of Land and Architectural Studies (UCLAS-Ardhi University) , Mbeya Institute of Technology (MUST) naWater Development& Management Institute. 

Mpango huu unafadhiliwa na TEA kupitia mchango unaotolewa na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC). TCC Wamechangia kufadhili mpango huu kwa miaka mitatu kwa awamu ya kwanza yaani mwaka 2011/12, 2012/2013 na mwaka huu wa 2013/14.  Ambapo kwa miaka miwili wamechangia shilingi Milioni 300. 

MPANGO ENDELEVU KUFADHILI MAFUNZO HAYA
TEA itaendelea kutafuta wafadhili kwa ajili ya kufadhili program hii. TEA inaamini kuwa mafunzo haya yatasaidia kuongeza idadi wataalamu wa kike katika sayansi.
Aidha TEA itaingia makubaliano ya miaka mitatu na TCC kwa awamu ya pili kuanzia januari, 2014 ili kutoa ufadhili kwa mafunzo hayo kwa vyuo vya ufundi. Katika awamu ya pili TCC imepanua wigo wa ufadhili na kukubali kutoaƬscholarshipƮkwa wanafunzi watakaofaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya shahada.

Katika mpango huu TEA hugharamia, malipo kwa wakufunzi, chakula na malazi kwa wanafunzi, Ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na gharama za kuratibu programu.Gharama ya kwa mwanafunzi mmojani wastani wa shilingi milioni moja (TShs 1,000,000).

WITO 
Mamlaka ya Elimu Tanzania inapongeza Vyuo vya ufundi vinavyoendesha mafunzo haya na inajizatiti kuendelea kutoa ufadhili. Aidha tunawahimiza wanafunzi we kike chukua masomo ya sayansi.Na kipekee tunatoashukrani kwa TCC kwa kuona umuhimu wa kusaidia serikali kuongeza wataalamu wa kike katika fani ya sayansi.  

Bibi. Sylvia Lupembe 
Meneja Habari Elimu na Mawasiliano, Mamlaka ya Elimu Tanzania. 

No comments:

Post a Comment