TANGAZO


Friday, October 11, 2013

Vijana wafurahia uwepo wa Kampuni ya GODTEC Iringa


Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Joyce Mwakisyala akifafanua jambo kwa wadau waliotembelea Banda la Kampuni ya GODTEC(T) LTD  katika maonesho ya wiki ya Vijana yanayoendelea mkoani Iringa.

Meneja Masoko wa Kampuni ya GODTEC Bwana Thomas Munasi akielezea namna Kampuni yao inavyo wasaidia vijana kutengeza ajira kwa kuanzisha makampuni walipotembelea banda la kampuni hiyo katika wiki ya maadhimisho ya wiki ya vijana ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Iringa.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. A. S. Mwamwindi akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Mfumo wa Utajirishaji unaoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Kampuni ya GODTEC na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alipotembelea banda la Kampuni hiyo jana katika maonesho ya wiki ya Vijana yanayoendelea mkoani Iringa,kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sparke Intertional ambayo ni zao la mfumo huo Bwana Gerald Magooge Reuben.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya BRECO Anthony Mwambanga akifafanua jambo kwa wadau wa vijana waliotembelea banda la Kampuni ya GODTEC wakati wa maonesho ya wiki ya vijana inayoendelea mjini Iringa. Breco ni Kampuni iliyotokana na mfumo wa utajirishaji unaoratibiwa na GODTEC.

Wadau wa vijana wakipata maelekezo kutoka kwa Maofisa wa Kampuni ya GODTEC walipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya wiki ya vijana mjini Iringa. (Picha zote na Frank Shija - WHVU)

No comments:

Post a Comment