Shirika la Amnesty International limesema rekodi ya Saudi
Arabia kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu inazidi kuwa mbaya.
Shirika hilo limesema nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta haijashindwa tu
kutekeleza mabadiliko iliyoahidi Umoja wa Mataifa miaka minne iliyopita, bali
limesema imeongeza ugandamizaji.Uingereza imependekeza mageuzi ya mfumo wake ya wanaume kua walinzi wa wanawake.
Pendekezo hili liliungwa mkono na Marekani iliyozusha kashfa ya wafanyakazi wa kigeni wanaolimbikiziwa kazi za kupinduukia katika mazingira yasiyokubalika na kwa shurti.
Taifa hilo la Kiarabu limetuhumiwa kwa kuwafunga wanaharakati wa mageuzi bila kupitia mchakato wa sheria pamoja na kukiuka haki za msingi za wanawake na wafanyakazi wa kigeni.
Ujumbe wa Marekani pia ulitoa hoja kuhusu masharti makali yanayowekwa juu ya haki za kuabudu na Uhuru wa mihadhara, huku Ujerumani ikiongezea sauti yake kwa kutaka Ufalme huo urekebishe sheria yake ya adhabu ya kifo.
Rais wa tume ya haki za binadamu ya Saudi Arabia, Bandar bin Mohamed Al Aiban alisema kua Ufalme wa Saudi Arabia, ambao una wafanyakazi milioni 9 wa kigeni kati ya raia wake milioni 28 inajitahidi kulinda haki zao na vilevile kuweka mazingira yanayostahili.
Miongoni mwa hatua zinazochukuliwa hivi sasa ni marufuku kwa mfanyakazi kufanya kazi nje ya jengo wakati wa majira ya joto kipimo cha jotop kinapopanda sana.
Bw.Bandar amesema kua Sharia ya Kislamu kwayo haibagui baina ya wanawake na wanaume kwa sababu inachagiza usawa baina ya jinsia bila kubagua na kua sheria za dola hazibainishi tofauti ya wanaume wala wanawake, alisema Bw.Bandar.
Aliongezea kusema kua wanawake wa Saudi Arabia ni raia wenye haki sawa na kamili wenye haki ya kumiliki mali bila kuomba ruhusa kutoka popote.
Uingereza ilisema kua wanawake wanastahili kupewa fursa katika uongozi na mamlaka zaidi na kuitaka serikali ya Saudi Arabia ikomeshe mfumo wa kuwalinda raia hususan wanawake.
Baadhi ya sheria zinazowakwaza wanawake ni haki zao katika ndoa, talaka, watoto, urithi, kumiliki mali na maamuzi yoyote katika familia.
No comments:
Post a Comment