Watu watatu akiwemo msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8
aliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami wakiwa kwenye pikipiki kushambulia
sherehe za ndoa nje ya kanisa la Kikopti mjini Cairo.
Takriban wengine 9 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo mjini Giza.Jamii ya wakristo wa kikopti wamekuwa wakishambuliwa na baadhi ya waisilamu wanaotuhumu kanisa kwa kuunga mkono jeshi katika kumpindua aliyekuwa Rais Mohammed Morsi mwezi Julai.
Washambuliaji hao ambao hawakutambuliwa, waliwafyatulia risasi kiholela watu waliokuwa wanaondoka kanisani.
Mwanamume mmoja na mtoto huyo waliuawa nje ya kanisa hilo wakati mwanamke mmoja akifariki akipelekwa hospitalini.
"Tulisikia mlio mkubwa sana mfano wa kitu kilichokuwa kinaanguka,’’ alisema shahidi mmoja.
"Nilimkuta mwanamke mmoja akiwa ameketi kwenye kiti chake, akiwa amejeruhiwa kwa risasi. Watu wengi walikuwa wameanguka kando yake akiwemo mtoto mdogo.’’
Kasisi wa kanisa hilo Thomas Daoud Ibrahim alisema kuwa alikuwa ndani ya kanisa hilo, wakati, milio ya risasi ilikuwa inasikika.’’
"Kilichofanyika ni kitu kibaya sana na sio waksristio wakopti waliolengwa pekee yao , tunaharibu nchi yetu,’’ alisema kasisi huyo.
Kasisi mwingine aliambia vyombo vya habari kuwa kanisa hilo liliachwa bila polisi wala mlinzi tangu mwishoni mwa mwezi Juni.
Kanisa hilo ni moja ya makaisa ya zamani ya kikristo iliyoanzishwa mjini Alexandria mapema miaka ya 50 AD.
Idadi ya wakristo nchini Misri ni asilimia 10 ikiwa waumini milioni 80, na wamekuwa wakiishi kwa amani na waisilamu wa kisunni kwa miaka mingi.
Hata hivyo, kuondolewa mamlakani kwa Morsi kijeshi, kumefuatiwa na mashambulizi mabaya dhidi ya makanisa na rasilimali za waumini hao kwa miaka mingi.
Wakati mkuu wa majeshi Generali, Abdul Fattah al-Sisi, alitangaza kwenye televisheni kuwa rais Morsi aliondolewa mamlakani baada ya maandamano makubwa yakimtaka ajiuzulu aliandamana na papa Tewadros.
Tewadros alisema kuwa mkakati uliofikiwa na Al-asisi ulitokana na mawazo ya viongozi waheshimiwa ingawa hakuwataja.
No comments:
Post a Comment