TANGAZO


Monday, October 21, 2013

Zaidi ya 40 wauawa na waasi Jonglei

 


Jeshi linasema ni washambuliaji wanaaminika kuwa waasi
Zaidi ya watu 40 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, katika shambulizi dhidi ya vijiji katika jimbo la Jonglei nchini Sudan kusini
Msemaji wa jeshi ameelezea kuwa washambuliaji wanaaminika kutoka katika kundi la waasi la David Yau Yau. Jimbo la Jonglei limeathirika sana kutokana na makabiliano ya kikabila na mizozo kuhusu ardhi na umiliki wa mifugo.

Zaidi ya watu 1,500 wanakadiriwa kuuawa kayika jimbo hilo tangu Sudan Kusini kujitawala mwaka 2011.
Maelfu ya wengine wameachwa bila makao kufuatia mapigano hayo.
Msemaji wa jeshi, Kanali Philip Aguer, ameambia BBC kuwa angalau nyumba katika vijiji viwili ziliteketezwa wakati wa shambulizi hilo Jumapili.
Wapiganaji hao, walijihami kwa budnduki na rketi za RPG wakati wa mashambulizi.
Maelfu ya mifugo pia waliibwa wakati wa mashambulizi hayo, kwa mujibu wa Gavana wa jimbo la Jonglei, Hussein Maar, .

Sudan Kusini inakubwa na tatizo la kusambaa kwa sila ndogondogo zilizotokana na miaka mingi ya vuta dhidi ya utawala wa Khartoum.
Hata hivyo Serikali ya Sudan ilikubali kuipa Uhuru Sudan ksuini tangu mwaka 2011 baada ya mazungumzo ya amani yaliyoongozwa na Marekani pamoja nan chi zengine za kikanda.

Mifufo ndio njia kubwa ya kujikimu kimaisha kwa wenyeji wananchi wa taifa hilo, ambayo haina benki nyingi na hutumiwa kulipa mahati pamoja na kutumiwa kama chakula wakati wa msimu wa kiangazi.
Ng’ombe mmoja anaweza kugharimu dola nyingi kulingana na rangi yake.

No comments:

Post a Comment