TANGAZO


Monday, October 7, 2013

Rais Kikwete kuongoza kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha wakunga

Mkurugenzi wa Shirika la AMREF Tanzania, Dk. Festus Ilako (katikati), akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu chakula cha hisani cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga, kupitia kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania” siku ya Ijumaa Oktoba 11, mwaka huu. Mgeni rasmi katika hafla hiyo, atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete ambaye ataongoza uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kampeni hiyo. Kushoto ni Mkurgenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage, Teddy Mapunda na kulia ni Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline Woiso.
Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline Woiso (kulia), akisisitiza jamii nzima juu ya kutambua umuhimu wa kuwasomesha wakunga nchini ambapo azma hiyo, itafanikiwa kwa kuunga mkono kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la AMREF Tanzania, Dk. Festus Ilako.
Mkurgenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage, Teddy Mapunda (kushoto), akiwashukuru washirika wanaoendelea kuunga mkono kameni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”, baadhi ya washirika hao ni ITV/Radio One, Clouds Media Group, Banki Kuu Tanzania (BOT), Serena hoteli, benki ya NBC, Toyota Tanzania Tanzania One, DSTV, PPF, TACAIDSWHO na MSD. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la AMREF Tanzania, Dk. Festus Ilako.
Baadhi ya waandishi wa habari na washiriki wa mkutano unaohusu chakula cha hisani cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga uliofanyika wakiwa katika hafla hiyo leo, jijini Dar es Salaam. Kampeni ya kuchangisha fedha inaongozwa na kauli mbiu inayosema “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”. Chakula hicho cha hisani kitafanyika siku ya Ijumaa Oktoba 11, mwaka huu, Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, ambaye ataongoza uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kampeni hiyo. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment