Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Productions, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS), Rita Poulsen (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maendeleo ya shindano hilo, huku akiwataka wadau kuwapigia kura washiriki 12, waliofikia hatu ya mwisho ya shindano hilo. Kushoto ni Mtaalamu Huduma za ziada wa Kampuni ya simu ya Zantel, Mhina Cecil na kulia ni Meneja wa Huduma wa kampuni ya Zantel, Haji Yussuf Ramadhan.
Juu na chini washiriki hao, wakiimba wakati walipokuwa wakijitambulisha kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Juu na chini washiriki hao, wakiimba wakati walipokuwa wakijitambulisha kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Mshiriki wa Epiq Bongo Star Serch, Elizabeth Mwakijambile, akiimba mmoja ya nyimbo zake, alipokuwa akijitambulisha kwa waandishi wa habari, ukumbi wa Mgahawa wa City Sport & Lounge, Dar es Salaam leo, wakati Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Productions, ambaye pia ni Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search, Rita Poulsen (kulia), alipokuwa akielezea kuhusu maendeleo ya shindano hilo, huku akiwataka wadau kuwapigia kura washiriki 12, waliofikia hatu ya mwisho ya shindano hilo. Katikati ni Mtaalamu wa Huduma za ziada wa Kampuni ya simu ya Zantel, Mhina Cecil.
Mtaalamu Huduma za ziada wa Kampuni ya simu ya Zantel, Mhina Cecil, akizungumza katika hafla hiyo jijini leo.
Meneja wa Huduma wa Kampuni ya Zantel, Haji Yussuf Ramadhan, akizungumza katika hafla hiyo leo.
Washiriki, viongozi wa EBSS na wa Kampuni ya Zantel wakiimba moja ya wimbo wa kuisifia BBS, wakati wa hafla hiyo, ukumbi wa mgahawa wa City Sport & Lounge, jijini Dar es Salaam leo.
Na Asha Kigundula
FAINALI za mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba ya Epiq Bongo Star Search (EBSS), mwaka huu 2013, zitafanyika Novemba 17, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano maalum na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Productions, Rita Poulsen, alisema kuwa maandalizi ya fainali hizo, yanaendelea vizuri.
Poulsen alisema kuwa wamejipanga kuboresha mashindano hayo, na wadau watarajie kushuhudia fainali zilizoandaliwa katika kiwango cha bora cha Kimataifa.
Shindabo hilo, limeingia katika hatua ya mwisho ya wiki hii, ikiwa imebakisha washiriki 12, kuelekea katika kumpata mshindi wake atakayejinyakulia kitita cha Sh. milioni 50.
Alisema kuwa, awali walipata washiriki 50 lakini sasa baada ya kuwachuja wamebaki 12, ambao wapo kambini na kupewa mafunzo mbalimbali ya muziki kabla ya kuwachuja na kubaki wanane watakaoingia fainali.
"Hatua hii ni muhimu sana, hasa kwa kuwa inarudisha shindano kwa wananchi ili waweze kumchagua mshindi wao, hivyo naomba wawapigie kura kwa wingi washiriki wanaowapenda"alisema Poulsen.
Alisema katika shindano la mwaka huu, washiriki waliochaguliwa kwa usaili wa simu, nao waliungana na wenzao waliongia katika kumi bora wiki hii na kuonyesha uwezo mkubwa.
Poulsen alisema katika shindano la mwaka huu, ubora wa washiriki, ni mzuri, wamepata mafunzo wanayopata ndani ya Jumba la Epiq BSS ni kubwa hivyo, mashabiki watarajie mchuano mkubwa wa kuwania sh.milioni 50.
Washiriki waliyoingia hatua hiyo ni pamoja na Amina Chibaba, Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya, First Godfrey, Francis Vlavian, Furaha Charles, Furaha Mkwama, Joshua Kahoza, Maina Thadei, Mandela Nicholaus, Melisa John na Raymond John.
Naye Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema wamejipanga kuhakikisha shindano hilo linakuwa la aina yake mwaka huu kupitia udhamini wa Kampuni yake.
Alisema kuwa wananchi wawapigie kura washiriki wanaoamini ni wazuri na watafanya vizuri katoka soko la muziki.
"Maana ya kufungua laini za watu kupiga kura mapema ni kuwapa nafasi ya kuchagua mshindi wampendae, na wanaweza kupiga kura hata kwa washiriki zaidi ya watatu", alisema Khan.
Alisema pia bado washiriki wanaendelea kusailiwa kupitia namba ya simu 0901551000 au kutuma ujumbe mfupi kwenda 15530.
No comments:
Post a Comment