TANGAZO


Monday, October 7, 2013

Matukio mbali mbali ya Uhamiaji Sports Club ilivyoshiriki fainali za mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma.


*Yanyakua ushindi wa nne kuvuta kamba

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Rehema Nchimbi (kushoto), akikagua timu ya kuvuta kamba ya Uhamiaji kabla ya fainali na timu ya Ikulu.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kushoto), akikagua
timu ya kuvuta kamba ya Uhamiaji kabla ya fainali na timu ya Ikulu.
Timu ya kuvuta kamba ya Uhamiaji ikimenyana na timu ya Ikulu (haipo pichani), katika fainali za mashindano
ya SHIMIWI yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma.
Timu ya kuvuta kamba ya Ikulu  ikimenyana na timu ya Uhamiaji (haipo pichani) katika fainali za mashindano ya Shimiwi, yaliyofanyika mwishoni  mwa wiki mjini Dodoma.
Watumishi wa Uhamiaji wakiwa katika maandamano ya kufunga mashindano ya SHIMIWI mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
 Viongozi waandamizi serikalini wakipokea maandamano ya kufunga rasmi mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma  mwishoni mwa wiki.
Watumishi wa Uhamiaji wakiwa katika hafla ya kujipongeza baada ya kunyakua ushindi wa nne katika uvutaji kamba katika mashindano ya  SHIMIWI, mjini Dodoma.
Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ambokile Sylvester akiongea na watumishi wa Idara yake wakati wa hafla ya kuwapongeza kwa kushiriki vizuri mashindano ya SHIMIWI. Hafla ilifanyika ukumbi wa St.Gaspar mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Watumishi wa Uhamiaji wakiserebuka wakati wa hafla ya kujipongeza kwa kushiriki vizuri mashindano ya SHIMIWI iliyofanyika ukumbi wa St. Gaspar mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment