TANGAZO


Tuesday, October 15, 2013

Mwili wa Mama yake mwandishi na mtangazaji wa ITV, Ufoo Saro, ukitolewa Chumba cha Maiti cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwenda kuagwa nyumbani kwao Kibamba

Jeneza lenye mwili wa mamake mzazi wa Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro, marehemu Anastazia Peter Saro, likiwekwa kwenye gari leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa ajili ya kupelekwa nyumbani kwao, Kibamba jijini, kuagwa tayari kusafirishwa kwa maziko nyumbani kwao Arusha. Ufoo na mamake walipigwa risasi na mpenzi wake Ufoo, kitendo ambacho kilisababisha mauti kwa mama huyo na Ufoo kujeruhiwa tumboni. (Picha zote na Khamisi Mussa)

Mtangazaji wa ITV, Sam Mahela, akiwa kazini wakati wa kuchukuliwa mwili wa mama yake, Ufoo Saro, Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam leo.
Jeneza lenye mwili huo, likipakiwa kwenye gari tayari kupelekwa Kibamba kuagwa.

Gari lenye mwili huo, likiwa tayari kwa safari ya kuelekea Kibamba.

No comments:

Post a Comment