Bendi ya Kalunde, ikitumbuiza kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Amrefu kwa uratibu wa Kampuni ya Montage, Dar es Salaam hivi karibuni kwa ajili ya kuchangia Mwanamke wa Afrika. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Makamu wa Rais, Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwasili kwenye hafla ya chakula hicho cha jioni huku akisindikizwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Montage, Teddy Mapunda (kushoto), ikiyoratibu chakula hicho, Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya akinamama kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (kulia), akwa kwenye hafla hiyo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Teddy Mapunda (kushoto), waratibu wa hafla hiyo.
Mama Aisha Bilal, akiwa na Mama Tunu Pinda, wakiwa katika hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi, alikuwa Makamu wa Rais, Mohammed Gharib Bilal.
Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Montage, wakiwa katika hafla hiyo.
Makamu wa Rais, Mohammed Gharib Bilal, akikabidhiwa mfano wa hundi ya sh. milioni 25 na Maofisa wa Benki ya NBC kwa ajili ya kuchangia Mama wa Afrika katika kampeni iliyopachikwa jina la 'Stand Up for African Women'
Makamu wa Rais, Mohammed Gharib Bilal, akitoa vyeti kwa wadau waliofanikisha kwa njia moja ama nyingine katika kuchangia Mama wa Afrika. Hapa akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa AMREF, Omar Issa. Wa pili kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Issa.
Wadau wakipata chakula katika hafla hiyo.
Wadau wakijaptia msosi uliokuwa ukipatikana katika hafla hiyo.
Mtaalamu wa magonjwa ya akinamama, akitoa ushuhuda jinsi alivyojitolea katika kumsaidia mama aliyekumbana na matatizo katika uzazi na yeye kujitolea kwa juhudi zake zote katika kuokoa maisha yake mama huyo.
Maofisa wa Benki ya NBC, wakisikiliza maelezo kutoka kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment