TANGAZO


Wednesday, October 9, 2013

Mikutano ya Mwala ya Shirika la Fedh la Kimataifa na Kundi la Benki ya Dunia yaanza Washington DC



Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dk. Philip Mpango, Naibu Gavana wa BOT, Bi. Natu Mwamba na Mchumi wa Benki Kuu, Bi. Sauda Msemo  wakisikiliza kwa makini.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. Wiliam Mgimwa (kushoto), Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula wakimsikiliza  Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Dk. Silvacius Likwelile akitoa ufafanuzi.
Waziri wa Fedha Mhe. Dk. Wiliam Mgimwa akiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania kuhusu maandalizi ya mikutano na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Ujumbe wa Tanzania katika majadiliano, kutoka kushoto ni Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Mwanaidi Mtanda, Kamishna Idara ya Sera, Bw. Beda Shallanda, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT, Dk. Joseph Masawe na Bw. Said Magonya, Kamishna wa Fedha za Nje akielezea jambo.
Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Mhe. Yusuph Mzee (kulia), akisoma kwa makini taarifa zitakazowasiliswa katika mikutano hiyo mbele ya ujumbe kutoka Tanzania.
Toka kushoto ni Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. Wiliam Mgimwa, Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Silvacius Likwelile, Mkurugenzi wa Idara ya kupunguza Umasikini (MKUKUTA), Bi. Anna Mwasha pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya  wakisikiliza kwa makini.
Ujumbe wa Tanzania wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na Waziri wa Fedha hayupo pichani ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho.
Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dk. Philip Mpango, Naibu Gavana wa BOT, Bi. Natu Mwamba na Mchumi wa Benki Kuu Bi. Sauda Msemo  wakisikiliza kwa makini.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. Wiliam Mgimwa (kushoto), Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula wakimsikiliza  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Silvacius Likwelile akitoa ufafanuzi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dk. Wiliam Mgimwa akiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania kuhusu maandalizi ya mikutano na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Kushoto ni Kamishna wa Idara ya Sera, Bw. Beda Shallanda akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT, Dk. Joseph Masawe.
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula akimsikiliza kwa makini Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, Bw. Paul Mwafongo. (Picha zote na Bi. Eva Valerian – Washington DC)



 Mikutano ya mwaka ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2013 imeanza rasmi leo mjini Washington D.C. Mikutano hii itafikia kilele chake hapo tarehe 11 – 13, mwezi Octoba ,2013.  

Bodi ya Magavana wa kundi la Benki ya Dunia ( Benki ) na Bodi ya Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( Mfuko) kwa kawaida hukutana mara moja kwa mwaka kujadili kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama. 
Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe. Dk. Willium Mgimwa , Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvanus Lekwilile pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu wao ni Magavana wa mikutano hiyo. Nchi karibu zote zimeshawasili katika mikutano hii. 
  
 ‘Lengo la mikutano hii kwa nchi ya Tanzania, inatupa nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi.  

"Nia yao kubwa ni kutusaidia na kusikia tuna mawazo gani na maeneo gani wanaweza wakatusaidia katika kuboresha na kuangalia kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri’. amesema  Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa alipokuwa akijadiliana na ujumbe kutoka Tanzania.  


 Aidha Mhe. Dkt. Mgimwa alisema kuwa, Katika mazungumzo na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa, ujumbe wa Tanzania utawasilisha hali halisi ya utendaji wa kiuchumi wa Tanzania na hali ya matumizi na mapato ya fedha na mambo yanayohusiana na taasisi zinazoendesha nishati kama vile Shirika la umeme Tanazania (Tanesco) na shirika la maendeleo ya mafuta Tanzania (TPDC) pamoja na kutazama mienendo ya madeni yetu na mwenendo wa mapato kwa ujumla.


Hali ya hewa mjini hapa ni ya manyunyu na mvua za hapa na pale.

Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
Washington D.C
7/10/2013

No comments:

Post a Comment