Mbunge
wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati (kushoto), akimkabidhi Katibu
Mtendaji wa Klabu ya Waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa (IPC), Francis Godwin
msaada wa kompyuta kwa ajili ya mradi wa IPC VICOBA, unaoendeshwa na IPC, mkoani humo leo. (Picha na Francis Godwin Blog)
Na
Francis Godwin, Iringa
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati, ametimiza ahadi yake ya madawati 100, vitabu kwa shule za Msingi na Sekondari pamoja na kompyuta moja kwa klabu ya waandishi wa habari mkoani Iringa (IPC)
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati, ametimiza ahadi yake ya madawati 100, vitabu kwa shule za Msingi na Sekondari pamoja na kompyuta moja kwa klabu ya waandishi wa habari mkoani Iringa (IPC)
Akikabidhi
ahadi hiyo leo, Kabati alisema kuwa amelazimika kutimiza ahadi hiyo ili
kupunguza sehemu ya ahadi mbali mbali ambazo alipata kuwaahidi wananchi wa
jimbo la Iringa mjini pamoja na zile ambazo aliombwa na wanahabari mkoa wa
Iringa ili kusaidia kuongeza vitendea kazi kwa ofisi ya wanahabari mkoani
hapa.
Kabati
alisema kuwa madawati hayo 100 aliyokabidhi ni kwa shule za msingi nane za
jimbo la Iringa mjini na vitabu ni kwa ajili ya shule za sekondari 5 za jimbo
la Iringa mjini.
Mbunge
huyo alisema madawati hayo yanathamani ya zaidi ya Tsh milioni 6 wakati
vitabu hivyo ameviomba kutoka kwa wadau wake kwa ajili ya kusaidia
kupunguza uhaba wa kiada na ziada katika shule za sekondari jimbo la Iringa
mjini.
Hata
hivyo alisema kuwa misaada hiyo amekuwa akiitoa mfukoni mwake na posho yake
anayoipata bungeni hasa ukizingatia yeye si mbunge wa jimbo ambae anapewa
bajeti ya kusaidia maendeleo ya jimbo kwa maana ya mfuko wa maendeleo wa
jimbo .
"
Mimi nimekuwa nikitumia posho zangu kusaidia maendeleo jimbo la Iringa
mjini hasa mkitambua kuwa mimi sina mfuko wa jimbo ila kama ningelikuwa
mbunge wa jimbo kero hizi zingetatuliwa kupitia mfuko wa jimbo.....ila
bado nahawakikishieni nitaendelea kuchangia maendeleo ya jimbo la Iringa
mjini"
Akielezea
juu ya msaada wake wa kompyuta kwa aliyoikabidhi kwa uongozi wa IPC Kabati
alisema kuwa mbali ya msaada huo wa Kompyuta bado ataendelea kuwasaidia
wanahabari Iringa ikiwa ni pamoja na kumwomba waziri wa habari , vijana
utamaduni na michezo Dr Fenella Mkangala ili ikiwezekano IPC kuendelea
kusaidia zaidi hasa kupitia IPC Vicoba mpango ambao umekuwa ukiwasaidia
wanahabari kupata mikopo nafuu
Kwa
upande wake mlezi wa IPC Salim Asas alimshukuru mbunge Kabati kwa kuendelea
kuwasaidia wanahabari na jamii nzima ya jimbo la Iringa.
Alisema
kuwa kinachofanywa na mbunge Kabati kinapaswa kuigwa na wabunge wengine
katika kuwasaidia wanahabari ila jamii inayowazunguka pia.
No comments:
Post a Comment