TANGAZO


Saturday, October 26, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal ashiriki sherehe za maadhimisho ya Siku Kuu ya Bugando na kuzindua jengo la matibabu ya Saratani na huduma za upasuaji wa moyo, mkoani Mwanza


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la matibabu ya Ugonjwa wa Saratani na Huduma za upasuaji wa Moyo, katika Hospitali ya Bugando Mkoa wa Mwanza, wakati wa wa Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini hapo. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto) akishuhudia zoezi la upasuaji wa Moyo alipokuwa akifanyiwa mmoja wa wagonjwa wa Moyo ndani ya Hospitali ya Bugando, baada ya kuzindua Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo, mkoani Mwanza leo wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini hapo.

Shughuli ya Upasuaji mgonjwa wa Moyo ikiendelea.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa kati ya watoto 18 waliokwishafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Bugando kwa gharama ya SH. 50, 000/ badala ya gharama sahihi ya Sh. milioni 6. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, leo amehudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini hapo na kuzindua Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo, mkoani Mwanza.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal (katikati) akionyeshwa moja ya mashine zinazotumika wakati wa upasuaji wa Moyo katika Hospitali ya Bugando. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando 'Bungado Day', iliyofanyika leo jijini Mwanza sambamba na uzinduzi wa Jengo la Matibabu ya Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishuhudia moja kati ya chupa ya mafuta ya Vaseline, ambayo ni 'Feki' yaliyokamatwa na TFDA, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye Sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Bugando, iliyofanyika leo sambamba na uzinduzi wa Jengo la matibabu ya Ugonjwa wa Saratani na Huduma za upasuaji wa Moyo. (Picha zote na OMR)

No comments:

Post a Comment