TANGAZO


Tuesday, October 8, 2013

Cheka apewa mwaliko kuhudhuria mapambano ya ngumi siku ya Idd Pili, Muheza mkoani Tanga


KOCHA wa mchezo  wa ngumi, Wilaya ya Muheza, mkoani  Tanga, Charles Muhilu  'Spinks', amempatia bondia Fransic Cheka Mualiko wa kwenda kuhamasisha mchezo wa ngumi siku ya Idd Pili ya Siku Kuu ya Idd El Hajj katika Viwanja vya Jitegemee, Muheza ambapo siku hiyo, kutakuwa na mapambano ya ngumi, ambapo anategemewa kuwepo kwake kutasaidia kuhamasisha vijana kuweza kusonga mbele na mchezo huo, ili hapo mbele waweze kufanya vizuri na kuliletea sifa Taifa kama alivyofanya yeye.

Akizungumza na Blog ya Super D, kutoka Muheza mkoani Tanga, Mhilu amesema "Unajua mimi namfundisha Cheka mazoezi ya ziada sasa hapa kwangu wanamsikia mimi namfundisha bingwa huyu, sasa nimeamua kumpa mwaliko ili aje hapa kwetu, watu wamuone kuwa ni yule Cheka aliyechukuwa Ubingwa wa WBF, kwa kumtwanga Mmarekani.

Mhilu alitoa rai kwa wadau wa mchezo huo, kujitokeza kusapoti mchezo wa ngumi kwa njia moja au nyingine kwa kuwa mchezo huo, unapendwa na vijana wengi wanaofanya  vizuri, inaweza kuwa ni ajira nzuri kwa vijana kama ilivyo kwa bonia Fransic Cheka, ambaye amekuwa akiwakilisha Mkoa wa Morogoro, ambapo kwa sasa yeye ni bingwa wa dunia 

"Pia alikaribishwa Bungeni, mjini Dodoma kushudia shughuli za Bunge na na Bunge la Jamhuri, alipotoka bungeni alipewa zawadi nzuri na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kwa kumpatia kiwanja pamoja na tani mbili za saruji pamoja na mabati kwa ajili ya kujengea nyumba, hivyo kwa kuchukuwa ubingwa huo, Cheka kumemuwezesha kupatiwa viwanja viwili kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kisasa na Serikali ya mkoa huo", alisema Mhilu.

No comments:

Post a Comment