TANGAZO


Tuesday, October 8, 2013

Taswira mbalimbali za kuanza Wiki ya Vijana Kitaifa mkoani Iringa

Viunga vya mji wa Iringa, ambao utakuwa Mwenyeji wa Wiki ya Vijana Kitaifa, kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013. 
Askari wa Kikosi cha Zimamoto, wakitoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa Iringa namna kutumia vifaa vya kuzimia moto na jinsi  ya  kukabiliana na majanga ya moto katika maeneo yao leo, wakati wa maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa waliofika katika banda la maonyesho la VETA, Iringa wakipata maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na na VETA kutoka kwa Oliva Adriano (katikati), mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika chuo cha Ufundi (VETA), Mkoa wa Iringa. 
Vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), Mkoa wa Iringa wakionyesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu wakati wa  Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa mkoani Iringa leo.
Baadhi ya watoto wakiangalia banda la Vijana kutoka mkoa wa Dar es Salaam na bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na Vijana hao leo, katika Viwanja vya Mlandege, mkoani Iringa. (Picha na Aron Msigwa -MAELEZO)

No comments:

Post a Comment