TANGAZO


Monday, September 30, 2013

WAMA: Saidieni watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

Meneja wa Mradi wa Pamoja Tuwalee kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Gloria  Minja, akizungumza jambo wakati wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha, Serikali, jamii na Sekta binafsi ili waweze kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu, chakula na malazi bora leo, jijini Dares Salaam.
Kaimu  Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Tabu Likoko, akifungua majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha, Serikali, Jamii na Sekta binafsi ili  waweze kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu, chakula na malazi leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mjumbe wa majadiliano hayo kutoka WAMA, Julius Jacob.
Mtaalamu  wa masuala ya ushauri katika mitaala, uandishi na uhariri, Victor Msinde (katikati), akichangia  mada juu ya   majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha, Serikali, jamii na Sekta binafsi ili waweze kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu, chakula na malazi leo, jijini Dares Salaam. Wengine ni wajumbe wamajadiliano hayo. (Picha zote Eleuteri Mangi –MAELEZO)

Na Magreth Kinabo – Maelezo
SEKTA binafsi na taasisi mbalimbali zimeshauriwa  kufadhili katika kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu badala ya kusaidaia matamasha pekee ikiwa ni hatua mojawapo ya  ya kuwapatia maisha bora, ikiwemo kupunguza umasikini  na tatizo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa  Mradi wa Pamoja Tuwalee kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Gloria  Minja wakati wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili  waweze kusaidia watoto hao.

“Tuzinaomba sekta binafsi  ikiwa ni moja wa wadau katika kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu katika malengo yao walijiwekea kupitia kipengele cha Uwajibikaji katika jamii (yaani corporate social responsibilities) kubadili mtanzamo wa kusaidia matamasha pekee ,bali waanze kufanya hivyo kwa watoto hawa ili nao waweze kusoma ,kutibiwa na kupata malazi,” alisema Gloria.

 Alisema ikiwa sekta hizo zitatekeleza wajibu huo, watoto hao wataweza kupata fursa ya kusoma , kupata kazi na kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ili waweze kuendesha maisha yao. 

 Gloria aliongeza kuwa mbali sekta hiyo , Serikali na   kila mwanajamii  wanawajibu  kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao , kwa kufanya hivyo kutasaidia  kuwawezesha kupata mahitaji muhimu  na kupunguza tatizo la umaskini  nchini.

 Akizungumzia  kuhusu ujumbe uliokuwa unatengenezwa na wadau hao kutoka sekta binafsi na Serikali alisema lengo lake litakuwa ni kutoa ushawishi kwa jamii nzima  ili iweze kuwatambua na kuwahudumia watoto hao.

 Aidha  alisema   ujumbe huo  utatumika  kuhamasisha katika kampeni ya utetezi  kwa watoto hao ili  Serikali, Jamii na sekta binafsi zitambue  kuwa jukumu la kuwalea watoto hao ni la pande zote. 

 Akifungua  majadiliano hayo Kaimu  Katibu Mtendaji wa  WAMA , Tabu  Likoko  alisema  kuwa  taasisi hiyo inafanya kazi ya kusaidia elimu kwa watoto wa kike, yatima na uwezeshaji kwa wanawake. 

Mradi huo wa Pamoja Tuwalee unatekelezwa katika mikoa  ya  Morogoro,Pwani, Dares Salaam na Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu,ambapo ulianza kutekelezwa mwaka 2011 hadi mwaka 2013 na WAMA  kwa ushirikiano wa fhi360 chini ufadhili wa Shirika  la Misaada la Marekani(USAID).

No comments:

Post a Comment