Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana (hawapo pichani), wakati wa hafla ya kumuaga na kumpongeza iliyoandaliwa na wafanyakazi wa idara hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kumuaga na kumpongeza. Profesa Gabriel kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu alikuwa Mkurugenzi wa Idara Maendeleo ya Vijana.
Ofisa Vijana Mwandamizi, Ernest Ntweneshe akitoa nasaha kwa niaba ya wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, mbele ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Hbari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabariel (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kumuaga na kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel ( kushoto), akipokea zawadi ya shati kutoka kwa wafanyazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, aliyokabidhiwa kwa niaba yao na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, James Kajugusi mapema mwishoni mwa wiki, katika hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto), akigonga chupa ili kutakiana heri na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wakati wa hafla ya kumpongeza kwa kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo. Kabla ya uteuzi huo Profesa Gabriel alikuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (waliokaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wakati wa hafla fupi ya kumpongeza na kumuaga. (Picha zote na Frank Shija - WHVUM)
No comments:
Post a Comment