Ofisa Habari wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Kassim Nyaki, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu utekelezaji wa mchakato wa Ajira katika sekretarieti hiyo. Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Idara ya Ajira wa ofisi hiyo, Aurelia Matagi na kulia ni Ofisa Habari Maelezo, Frank Mvungi.
Ofisa Habari wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Kassim Nyaki, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu utekelezaji wa mchakato wa Ajira katika sekretarieti hiyo. Kulia ni Ofisa Habari Maelezo, Frank Mvungi.

Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Ofisa Habari wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Kassim Nyaki, alipokuwa akizungumza kuhusu utekelezaji wa mchakato wa Ajira katika sekretarieti hiyo. (Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)
JUKUMU kubwa na la
Msingi la Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni kuendesha mchakato
wa ajira Serikalini. Tangu kuanza kwa majukumu yake Machi, 2010 hadi Juni,2013
imetangaza jumla ya nafasi za kazi zipatazo 8,535 ambapo jumla ya maombi 172,
936 yalipokelewa. Kati ya hizo nafasi 5,037 hadi kufikia mwezi Agosti, 2013
zilikuwa tayari zimejazwa na nafasi 2,291 ujazaji wake upo katika hatua
mbalimbali.
Ujazaji huo
umenyumbulishwa kwa jinsi na ngazi mbalimbali za elimu. Kati ya nafasi 5,037
wanaume walikuwa 2,836 sawa na asilimia 56.3%na wanawake walikuwa 2,201 sawa na
asilimia 43.7%. Wahitimu kutoka Vyuo vikuu ni 2,749 vyuo vya kati 1,999 na
wahitimu wa kidato cha nne (4) na sita(6) (supporting staff) ni 289.
Aidha kwa mwezi huu
wa Septemba,2013 jumla ya waombaji kazi wapatao 949 waliofanya usaili mwezi
Agosti wamepangiwa vituo vya kazi na wakati wowote majina yao yatawekwa kwenye
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira. Baada ya zoezi hili kukamilika tutakuwa
tumewashatuma kwa waajiri waombaji kazi 5,986 na kubakia na nafasi 1,342 ambazo
ujazaji wake upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Suala la pili ambalo ningependa kuliongelea ni
upangaji wa wahitimu wanaokwenda kufanya kazi katika maeneo ya pembezoni. Kwa
muda mrefu sana mikoa iliyopo pembezoni mwa Nchi yetu ilikosa watumishi wa
kutosha kutokana na vijana wengi wenye sifa waliokuwa wakipangwa kutopenda kufanya kazi katika maeneo hayo. Miaka ya
hivi karibuni Serikali imeboresha miundombinu pamoja na kuharakisha kwa
upatikanaji wa huduma muhimu na za
msingi katika maeneo mengi nchini.
Uboreshaji huo wa mazingira ya kazi pamoja na uhaba
wa ajira nchini kumeongeza mwamko kwa waombaji wengi wa fursa za ajira kupenda
kufanya kazi katika maeneo hayo ikiwemo Mikoa ya Mtwara, Lindi, Kigoma na
Rukwa. Kwa mfano tangu kuanza kwa sekretarieti ya Ajira mkoa wa Mtwara
tumepeleka watumishi wapya 234, Lindi watumishi 201, Kigoma watumishi 96 na
Rukwa na Katavi watumishi 122.
Mwamko wa waombaji wengi sasa hivi kupenda kufanya
kazi serikalini unajidhihirisha si tu kwa Sekretarieti ya Ajira kupokea maombi
mengi kila inapotangaza nafasi wazi za kazi bali pia kwa idadi kubwa ya wadau
wanaotembelea Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira. Tangu kuanzishwa kwake Aprili
2012 hadi kufikia jana imetembelewa na wadau zaidi ya 3,760,000.
Jambo la tatu ambalo ningependa kuzungumzia ni
kuhusu utumaji wa maombi ya kazi kwa njia ya mtandao (e-application). Kutokana
na changamoto nyingi zinazoendelea kujitokeza kwenye soko la ajira ikiwemo
wingi wa waombaji ambao unaleta ushindani mkubwa, ubora wa wahitimu na ukubwa
wa eneo la Nchi yetu kijiografia, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
inatarajia kufanya mabadiliko kwenye utaratibu mzima wa mchakato wa ajira
nchini ikiwemo utumaji wa maombi ya kazi kwa njia ya Kielectroniki
(e-application). Mfumo huu mpya utawawezesha
waombaji wa fursa za ajira kuwasilisha maombi ya kazi zitakazokuwa
zikitangazwa katika Utumishi wa Umma. Mfumo huo pia unalenga kuboresha mchakato
wa ajira ili waajiri waweze kupata waombaji wenye sifa kwa haraka zaidi.
Kabla
ya kumaliza nitoe wito kwa waombaji wa fursa za ajira ambao bado wana mtazamo
wa kuchagua maeneo ya kufanyia kazi, hususani wale wanaopangiwa vituo vya kazi
na Sekretarieti ya ajira na hawaendi kuripoti bila ya kutoa sababu za msingi
kuwa kwa sasa hawana sababu ya kufanya hivyo kama tulivyoeleza hapo awali na
kwa wale wanaofanya hivyo Sekretarieti ya Ajira inaandaa utaratibu wa
kutowaruhusu kufanya usaili mwingine.
Mwisho
nimalizie kwa kuwashauri
waombaji wa fursa za ajira na wale walioko shuleni kujikita zaidi katika masomo ya sayansi kwa kuwa kada hizo bado
zina upungufu wa wataalam ukilinganisha na fani za sanaa na biashara.
Imetolewa
na Kassim S. Nyaki, Afisa Habari, Ofisi
ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma +255-687624975. www.ajira.go.tz,
Facebook page ‘www.facebook.com/Sekretarieti Ajira’.
No comments:
Post a Comment