TANGAZO


Monday, September 30, 2013

Rais Kikwete na mkewe warejea nchini

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 wakitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda huku Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali akiangalia wakati alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 akitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa  Rombo Mhe Joseph Selasini wakati alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 akitokea Marekani katika ziara ya kikazi. Wanaofuatia ni Mbunge wa Nkenge Mhe. Asumpta Mshama na Mbunge wa Wawi Mhe Hamad Rashid Mohamed
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa  Viti Maalumu Mhe Rita Mlaki alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 akitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakilakiwa na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 wakitokea Marekani katika ziara ya kikazi. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment