Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania kutoka Ofisi Mitaa ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za (TAMISEMI), Mhandisi Nanai Nyariri, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Rebbeca Kwandu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapango wa uendelezaji Miji Tanzania katika mkutano uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa na kushoto ni Mratibu wa ULGSP, Boniface Nyiti.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kazini kwenye mkutano huo, wakati Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Rebbeca Kwandu, alipokuwa akieleza kuhusu mapango wa uendelezaji Miji Tanzania katika mkutano uliofayika leo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Rebbeca Kwandu, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mapango wa uendelezaji Miji Tanzania katika mkutano uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa na kulia ni Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania, kutoka ofisi hiyo, Mhandisi Nanai Nyariri.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Rebbeca Kwandu, akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu mapango wa uendelezaji wa Miji Tanzania katika mkutano uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Maendeleo Miji wa ofisi hiyo, Michael Mwalukasa na katikati ni Mratibu wa ULGSP, Mhandisi Boniface Nyiti.
Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania, Mhandisi Bonihace Nyiti, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, kuhusu mpango mkakati wa utekelezaji wa mradi huo ili kukabiliana na changamoto za miji. Wapili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Rebbeca Kwandu, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa na Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania, kutoka ofisi hiyo, Mhandisi Nanai Nyariri.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kazini kwenye mkutano huo, wakati Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Rebbeca Kwandu, alipokuwa akieleza kuhusu mapango wa uendelezaji Miji Tanzania katika mkutano uliofayika leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kazini kwenye mkutano huo, wakati Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Rebbeca Kwandu, alipokuwa akieleza kuhusu mapango wa uendelezaji Miji Tanzania katika mkutano uliofayika leo, jijini Dar es Salaam.
Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali
za maendeleo ya miji zikiwemo (i) ongezeko la watu kwa kasi mijini; (ii)
miundombinu isiyokidhi mahitaji ya miji; (iii) uwezo mdogo wa kifedha kwa ajili
ya kutoa huduma za jamii na (iv) usimamizi dhaifu wa maendeleo ya miji katika
Halmashauri zake. Inakisiwa kuwa hadi
mwaka 2030 asilimia 38 ya watu na takribani watu milioni 25 watakuwa wanaishi
katika miji.
Katika Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
wakati akifungua rasmi Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dodoma tarehe 30 Desemba 2005 alieleza juu ya dhamira ya Serikali katika
kuboresha miji yetu. Nanukuu
“Kuendeleza miji ni jambo
tutakalolipa uzito unaostahili ili tuwe na miji mizuri, safi na salama.
Serikali ya awamu ya Nne itazitaka Halmashauri zote zishughulikie jambo hili
haraka iwezekanavyo”.
Hivyo, kwa kutambua changamoto za miji zinazotukabili,
OWM-TAMISEMI ikishirikiana na wabia mbalimbali wa maendeleo, ikiwemo Benki ya
Dunia, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto hizo. Hatua hizo ni pamoja na kutekeleza miradi
mbalimbali. Miongoni mwa miradi ambayo
hivi sasa inatekelezwa na OWM- TAMISEMI ni mradi wa Uendelezaji wa Miji Mkakati Tanzania
ambao kwa kifupi unajulikana kama Tanzania Strategic Cities Project (TSCP) na Programu ya kuimarisha Halmashauri za Miji –
Urban Local Government Strengthening Programme (ULGSP). Aidha maandalizi ya Mradi wa Uendelezaji wa
Jiji la Dar es Salaam (DMDP) ambao ni mahsusi kwa Halmashauri tatu (3) za Dar
es Salaam nao yanaendelea
Mradi wa Uendelezaji wa
Miji Mkakati Tanzania-TSCP, ambao ni mkopo wa Banki ya Duniana DANIDA,
umegharimu Dola za kimarekani, Milioni 175.5, ambapo Dola Milioni 163.2 ni kutoka Benki ya Dunia na Dola Milioni 12.2
ni kutoka DANIDA. Mradi unatekelezwa katika miji 7 ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha,
Dodoma, Kigoma, Mbeya, Mtwara, Tanga na Mwanza. Kwa Dodoma mradi huu unatekelezwa
na Manispaa ya Dodoma na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA).
Mradi huu unalenga kuboresha Huduma za msingi katika
miji hii. Lengo hili litafikiwa kwa (i) Kuboresha Miundombinu kama barabara, maeneo ya kutupia taka ngumu, vituo
vya mabasi na malori na kununua vifaa vinavyosaidia kudhibiti taka ngumu (ii) Kuimarisha
uwezo wa kitaasisi katika uendelezaji na usimamizi wa Miji, Usimamizi na
Utunzaji wa mali za Halmashauri, usimamizi na ukusanyaji Mapato kutokana na
huduma muhimu za kijamii, uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato pamoja na
kuboresha mipango miji. Mradi huu ulianza kutekelezwa mwaka 2010 na unategemea
kukamilika mwaka 2015.
Programu ya
Kuimarisha Halmashauri (ULGSP) ambayo itafanyika katika miji 18 kwa lengo la kuziimarisha
Halmashauri katika maeneo Makuu Matano ili ziweze kutoa huduma bora zaidi kwa
wananchi kwa kuzingatia Sera ya Ugatuaji wa Madaraka(D&D) ambayo OWM-TAMISEMI
inatekeleza.
Maeneo
yanayolengwa katika mradi huu ni masuala ya (i) Uboreshaji wa Mfumo wa Mipango
miji, (iii) ukusanyaji wa mapato ya ndani hususani mapato yatokanayo na kodi ya
majengo, (iii) uboreshaji wa mifumo ya udhibiti fedha na manunuzi pamoja na
masuala ya mazingira na kijamii, (iv) uboreshaji wa mifumo ya utekelezaji,
uendeshaji na utunzaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma ya jamii pamoja na (v)
uboreshaji wa uwajibikaji na uwazi.
Mradi huu
unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kiasi cha Dola za Kimarekani 255 na
utatekelezwa katika Halmashauri za Miji 18 ya Tanzania Bara ambayo ni Iringa,
Moshi, Tabora, Lindi, Babati, Kibaha,Singida, Njombe, Mpanda, Sumbawanga, Geita,
Mpanda, Bariadi, Sumbawanga, Njombe, Musoma, Korogwe na Bukoba. Programu hii ilizinduliwa
na Mhe. Waziri Mkuu tarehe 18 Juni Mwaka huu wa 2013 ambapo utekelezaji wake
umeanza mwezi Julai, 2013 kwa kila Halmashauri kutangaza zabuni kwa ajili ya
usanifu wa miradi itakayotekelezwa.
Ufanisi wa
programu hii utavutia wadau wengine kushirikiana na Halmashauri nchini katika
kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.Pia itawezesha watakaotembelea Tanzania
katika siku zijazo kupata faraja na huduma bora. Programu
hii pamoja na miradi mingine inayotekelezwa itasaidia kubadilisha sura ya miji
ya Tanzania kwa kuifanya ivutie kwa uwekezaji, kuishi na kufanya kazi.
Akizindua programu hii mjini Moshi hivi karibuni, Mhe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda
alizitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa zinajenga tabia ya kutenga
bajeti kwa ajili ya kutunza miradi yote inayoanzishwa katika maeneo yao. Jambo
ambalo linaendelea kusisizwa na
OWM-TAMISEMI.
Benki ya
Dunia imeiteua Tanzania kuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kutekeleza Programu
hii kama mradi wa mfano na majaribio ambapo katika utekelezaji wake mfumo wa
kupima matokeo ya utekelezaji wa mradi ( Perfomance for Results) Utatumika.
Mradi huo
utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2013 hadi 2018 kwa
mkataba kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania, uliosainiwa mwezi
Desemba mwaka 2012 ambapo jumla ya Dola za kimarekani milioni 255 zimetengwa. Dola
milioni 201 kati ya hizo zitapelekwa moja kwa moja kwenye halmashauri na fedha
zinazobakia zitatumika katika suala zima la kujenga uwezo wa halmashauri kwa
kutekeleza mradi, pamoja na ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa programu.
IMETOLEWA
NA OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA
ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
No comments:
Post a Comment