TANGAZO


Wednesday, August 7, 2013

JUKWAA la Utamaduni la Wanadiplomasia wa Asia nchini Tanzania waandaa Tamasha la nane la filamu ('Asian Film Festival') jijini Dar es Salaam

Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Altaf Tajamul, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu tamasha la 8 la filam kwa nchi za Asia linalojulikana kwa jina la 'Asian Film Festival', litakalofanyika Agosti 14 hadi 23 mwaka huu kwenye jengo la Quality Centre, ukumbi wa Suncrest Cine Plex jijni. Kulia ni baadhi ya mabalozi na wanadiplomasia wa nchi hizo.
Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Altaf Tajamul, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu tamasha la 8 la filam kwa nchi za Asia linalojulikana kwa jina la 'Asian Film Festival', litakalofanyika Agosti 14 hadi 23 mwaka huu kwenye jengo la Quality Centre, ukumbi wa Suncrest Cine Plex jijni. Kulia ni baadhi ya mabalozi na wanadiplomasia wa nchi hizo.
Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Altaf Tajamul (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu tamasha la 8 la filam kwa nchi za Asia linalojulikana kwa jina la 'Asian Film Festival', litakalofanyika Agosti 14 hadi 23 mwaka huu kwenye jengo la Quality Centre, ukumbi wa Suncrest Cine Plex jijni. Kulia na kushoto ni baadhi ya mabalozi na wanadiplomasia wa nchi hizo.
Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Altaf Tajamul, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu tamasha la 8 la filam kwa nchi za Asia linalojulikana kwa jina la 'Asian Film Festival', litakalofanyika Agosti 14 hadi 23 mwaka huu kwenye jengo la Quality Centre, ukumbi wa Suncrest Cine Plex jijini. Kushoto ni baadhi ya mabalozi na wanadiplomasia wa nchi hizo.

Na Asmah Mokiwa

JUKWAA la Utamaduni la Wanadiplomasia Asia nchini Tanzania wameandaa maonesho ya nane ya filamu 'Asian Film Festival' yanayotarajia kuanza Agosti 14 hadi 23 mwaka huu kwenye jumba la sinema la Suncrest Cine Plex, Quality Centre, Dar es Salaam.

Mratibu wa maonesho hayo ambaye ni Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Tajammul Altaf alisema leo jijini kuwa lengo la maonesho ni kuonesha tamaduni za nchi za Asia nchini Tanzania.

Alisema balozi 10 za nchi za Asia nchini Tanzania zitaonyesha filamu zao zinazoonyesha tamaduni za nchi zao na kuongeza kuwa filamu hizo zitaanza kuoneshwa kuanzia saa moja usiku hadi saa tatu usiku.

Alisema lengo lingine ni kuendeleza uhusiano mzuri kati ya nchi za Asia na Tanzania, hususani katika masuala ya  kitamaduni.

Nchi hizo ni pamoja na China, India, Indonesia, Iran, Japani, Korea, Oman, Pakistani, Palestina na Vietnam.

Maonesho hayo yatafunguliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

Filamu zitakazoonyeshwa ni pamoja na filamu ya Khuda Kay Liye kutoka Pakistan, Swing Girls ya Japani, Scandal Makers kutoka Korea, Jaane Bhi Do Yaaro ya India, Habibie and Ainun ya Indonesia.

Nyingine ni The Maritime Silk Road ya Iran, Ocean Heaven kutoka China, Chuyen Cua PAO ya Vietnam, Five Broken Cameres ya Palestina na filamu ya Aseel ya Oman.

No comments:

Post a Comment