Msemaji wa Wakala wa Huduma za Ajira Bw. Peter Ugata (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jitihada zinazofanywa na wakala hiyo katika kuhakikisha wanakabiliana na changamoto za ajira nchini, katika mkutano uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa Huduma za Ajira kutoka Wakala wa Huduma za Ajira, Joseph Haule na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa na .
Mratibu wa Huduma za Ajira kutoka Wakala wa Huduma za Ajira, Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawamo pichani), kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kuzinduliwa rasmi mwaka 2008, wakati wa mkutano huo, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
1.0
UTANGULIZI
Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) ulianzishwa kwa Sheria Na. 30
ya mwaka 1997 (kama iliyorekebishwa mwaka 2009)
na kuzinduliwa rasmi tarehe 16 June, 2008 kufuatia Tamko la Serilkali Na.189 la
mwaka 2008. TaESA ilianza rasmi utekelezaji wa shughuli zake tarehe 1 Julai, 2008
ikichukua nafasi ya kilichokuwa Kituo cha Ajira nchini (Labour Exchange Centre).
Madhumuni ya kuanzishwa kwa
Wakala huu ni katika juhudi za Serikali kuona kuwa utoaji wa Huduma za Ajira
kwa umma unakuwa bora zaidi, wenye tija na wenye kuwafikia wananchi wengi
zaidi.
Wakala hutoa huduma zake kwa umma kupitia ofisi zake za
kanda zilizopo katika mikoa ya Dar es Salaam (Kanda ya Mashariki na Pwani), Mwanza
(Kanda ya Ziwa), Dodoma
(Kanda ya Kati) na Arusha (Kanda ya Kaskazini).
Dhima
“Kutoa
huduma bora za ajira katika sekta ya utumishi wa umma na binafsi kupitia
uunganishwaji watafutakazi, taarifa za soko la ajira kwa kuzingatia viwango
vinavyokubalika Afrika na kwingineko”.
Dira
“Kuwa
Wakala bora, imara na endelevu katika utoaji huduma za ajira katika sekta ya
utumishi wa umma na binafsi”.
2.0
SHUGHULI ZA WAKALA
-
Kuunganisha
watafutakazi na waajiri wenye fursa za ajira ndani na nje ya nchi.
-
Kuratibu
utoaji mafunzo ya ujuzi wa kazi na ushauri wa ajira.
-
Kuandaa
mipango ya utoaji huduma za ajira kwa waajiri, watafutakazi na wadau wengine.
-
Kukusanya,
kuchambua na kusambaza taarifa za soko la ajira.
-
Kuainisha
na kuzitambua Wakala binafsi zinazotoa huduma za ajira
-
Kuratibu
utoaji mafunzo yenye kulenga kuwapatia ujuzi wa kazi wanafunzi wanaosoma katika
shule za sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu.
2.1
UTEKELEZAJI
WA SHUGHULI ZA WAKALA
Katika kuhakikisha kuwa Wakala
unatekeleza Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008; Sheria ya Kukuza Ajira Na. 9
ya mwaka 1999 na katika hatua ya kukidhi matakwa ya Azimio Na. 88 la mwaka 1948
la Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambalo Tanzania imeliridhia, Wakala umeendelea
kutekeleza shughuli zake kwa njia zifuatazo:-
2.1.1
Kuwasajili
na kuwafanyia usaili wa awali watafutakazi
2.1.2
Kutembelea
waajiri ili kubaini fursa za ajira zitakazojazwa na watafutakazi waliosajiliwa
na wakala
2.1.3
Kutembelea
shule/vyuo ili kuwajengea uwezo wanafunzi ili kubaini hali halisi ya soko la
ajira na mahitaji yake.
2.1.4
Kuendesha
vipindi vya kuwajengea uwezo watafutakazi ili waweze kumudu ushindani na
changamoto za Soko la Ajira.
2.1.5
Kufanya
mikutano na wadau ili kupata maoni/mapendekezo yatakayofanikisha utekelezaji wa
majukumu ya Wakala.
2.1.6
Kushiriki
katika maonesho ya kitaifa na kimataifa kwa lengo la kujitangaza na kufikisha
huduma karibu zaidi na wananchi.
2.1.7
Kujitangaza
kupitia vyombo vya habari vikiwemo radio, televisheni na magazeti.
2.1.8
Kwa
kutumia Tovuti ya Wakala katika kutoa taarifa na kupata maoni ya wadau na umma kwa ujumla.
2.1.9
Kwa
kutumia ofisi zake za Kanda.
3.0
MAFANIKIO YA WAKALA
Tangu kuanzishwa kwake hadi
Juni, 2013 Wakala umefanikiwa katika
maeneo yafuatayo:-
3.1
Kuanzisha Ofisi za Kanda katika Mikoa ya Dare es
Salaam,
3.2
Wakala
umewahudumia jumla ya wateja 13,188 kati
yao
Watafutakazi 12,298,
waajiri 830 na
wakala binafsi 60
3.3 Wakala umeweza kusajili fursa za kazi 2,851 kwa kutembelea Waajiri 830
katika mikoa ya Shinyanga, Kagera,Mara, Mwanza, Singida, Tabora, Iringa,
Morogoro, Lindi,Arusha, Kilimanjaro na
Mtwara
3.4
Wakala
umeendesha vipindi kwa watafutakazi 1,426
kwa lengo la kuwajengea
uwezo
watafutakazi ili waweze kuhimili ushindani na
changamoto
za soko la ajira.
3.5
Watafuta
kazi 8,294 wamepewa ushauri juu ya
uchaguzi wa
fani, mafunzo ya kazi
zinazostahili kulingana na sifa zao ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri na
kuajirika.
3.6
Wakala
umeainisha Wakala Binafsi 60 zinazotoa
huduma za
ajira hapa nchini.
3.7
Kupitia
kitengo chake cha kuunganisha watafutakazi na
waajiri nje ya nchi, Wakala umeunganisha
watafutakazi 1,959 katika nchi za
UAE, Oman, India, Denmark na Saudi Arabia
3.8
Wakala
uko katika hatua za awali za kuwa na mfumo wa
kiteknolojia utakawezesha kukusanya na kusambaza taarifa za soko la
ajira.
3.9
Wakala
umeanzisha tovuti yake www.taesa.go.tz
ambayo
imetembelewa na wadau 440,230
ambao wametoa maoni na mapendekezo mbalimbali juu ya huduma zitolewazo na TaESA.
3.10
Wakala
umeweka utaratibu madhubuti wa kuratibu na
kusimamia uunganishaji wa Watanzania
kwenye soko la ajira nje ya nchi ili Watanzania waweze kupata kazi za staha na
kuepukana na biashara haramu ya usafirishaji watu “human trafficking”.
4.0
CHANGAMOTO
4.1
Kutokuwa
na rasilimali za kutosha kuwezesha kufikia malengo ya Wakala.
4.2
Kutokuwa
na fursa za kazi za kutosha ukilinganisha na idadi
ya
wahitimu/watafutakazi waliopo katika soko la ajira.
4.3
Watafuta
kazi wengi kuwa na matarajio makubwa kuliko hali halisi ya soko la ajira.
4.4
Baadhi
ya waajiri na watafutakazi kutotumia huduma za Wakala
5.0
MIKAKATI WA WAKALA KATIKA
KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO
Pamoja na changamoto zilizopo
wakala umepanga kufanya
yafuatayo:-
5.1 Kuendelea kuwaunganisha watafutakazi na
waajiri ndani na
nje ya nchi na kufanya utafiti katika nyanja za
upatikanaji
wa fursa za ajira.
5.2
Kukusanya,
kuchambua na kusambaza Taarifa za Soko la Ajira.
5.3
Kuendeleza
rasilimali watu ili kuongeza tija na ufanisi.
5.4
Kuendelea
kuainisha Wakala binafsi zinazotoa huduma za ajira nchini.
6.0
HITIMISHO
Lengo la kuandaa
taarifa hii ni kuwajulisha Watanzania na umma kwa ujumla kuhusu huduma
zitolewazo na Wakala kwa kuainisha sheria iliyoanzisha, shughuli za Wakala, utekelezaji
wa shughuli za Wakala, mafanikio, changamoto na mikakati ya kukukabiliana nazo.
Aidha, Wakala unachukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa kutupatia fursa
hii ya kuuelezea Wakala kwenu na Watanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment