TANGAZO


Friday, July 19, 2013

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara azindua 'Standard Chartered Goal Project'

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Liz Lloyd (kushoto) wakifuatilia maonesho ya ngoma kutoka kikundi cha Waanne Stars wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki. Mpango huo umelenga kuwajengea uwezo vijana hususan wanafunzi kujitambua, kujiamini na kulinda afya zao kwa kutumia michezo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanaki wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa ikioneshwa katika hafla ya uzinguzi wa Mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam. Mpango huo unafadhiliwa na Benki ya Starndard Chartered Tanzania.
Baadhi ya walimu wa michezo waliopatiwa mafunzo kwa ajili ya mpango huo wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa inaonyeshwa katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akicheza mpira wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki. Mpango huo umelenga kuwajengea uwezo vijana hususan wanafunzi kujitambua, kujiamini na kulinda afya zao kwa kutumia michezo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto), akiwa pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Liz Lloyd na Mkuu wa Shule ya Sekondari Zanaki, Rehema Funzo, wakielekea kwenye eneo la uzinduzi, ambapo Waziri Mukangara alikata utepe kuzindua rasmi Mpango wa Goal.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akikata utepe kuashiria Mpango wa Goal umezinduliwa rasmi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Liz Lloyd (kulia), wakifurahi baada ya kuzindua rasmi Mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Liz Lloyd wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa michezo waliokabidhiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo maalum kwa ajili ya mpango wa goal jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Liz Lloyd wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa michezo waliokabidhiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo maalum kwa ajili ya mpango wa goal jana jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija - Maelezo)

No comments:

Post a Comment