TANGAZO


Thursday, July 18, 2013

Waandishi wa Tanzania washerehekea miaka 95 ya Mzee Mandelea

Keki iliyoandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO  kwa ajili  ya kuadhimisha miaka 95 ya  kuzaliwa  Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee  Nelson Mandela. (Picha zote-Hassan Silayo – Maelezo)
Ofisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari - Maelezo, Anna Itenda, akitoa maelezo mafupi, jijini Dar es Salaam leo, jinsi alivyofanyakazi na Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela pamoja  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere. Kushoto  ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo, Zamaradi Kawawa. 
Ofisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari - Maelezo, Anna Itenda, akikata keki wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa kwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson. Keki hiyo iliandaliwa na Idara ya Habari- Maelezo.


Ofisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari-Maelezo, Anna Itenda  akimlisha keki Ofisa Habari Mwandamizi wa Idara hiyo, Jovina Bujulu, wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson  Mandela, huku waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali  wakifurahia tendo hilo, keki iliyoandaliwa na Idara ya Habari- Maelezo.

No comments:

Post a Comment