TANGAZO


Thursday, July 18, 2013

Tanzania yapokea mkopo wa shilingi Bil. 87 za ujenzi wa vituo vya kuhifadhia Vitambulisho vya Taifa


Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Saada Salum Mkuya (wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira A. Silima, wakipiga makofi ya shukrani baada ya Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa kusaini mkataba wa mkopo wa kujenga vituo vya kuhifadhia vitambulisho vya Taifa kutoka Export and Import Bank ya Korea, jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa na Mwenyekiti na  Rais wa Benki ya Export Import ya Korea, wakiangalia mikataba ya mkopo baada ya kusaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Elizabeth Nyambibo (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani, Mbaraka Abdulwakil (katikati) na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, wakifuatilia hafla ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhia vitambulisho vya Taifa  uliotolewa na Benki ya Export and Import Korea leo, jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa (kushoto), akiwa na Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export Import ya Korea  wakionyesha mkataba wa mkopo wenye thamani ya shilingi billioni 87 za  Kitanzania, waliosaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa (kushoto), akimpa mkono wa shukrani Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export Import ya Korea, wakati wakibadilishana hati za mkopo baada ya kusaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo, jijini Dar es Salaam. 


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Dickson Maimu (wa tatu kushoto) na Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import ya Korea, Yong Hwan Kim (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo, mara baada ya halfa ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhia vitambulisho vya Taifa leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (wa pili kushoto), Balozi wa Korea nchini, Chung Il (wa kwanza kulia), Mwenyekiti na Raisi wa Benki ya Export and Import ya Korea Yong Hwan Kim (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Saada Mkuya Salum (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kusaini mkataba wa mkopo wa kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa kutoka Benki ya Export and Import ya Korea.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa na Mwenyekiti na  Rais wa Benki ya Export Import ya Korea, wakisaini  mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwa Mwenyekiti na Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea, baada ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwa Mwenyekiti na Rais  wa Benki ya Export Import ya Korea, baada ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export and Import ya Korea, baada ya hafla ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhia vitambulisho vya Taifa, iliyofanyika Wizara ya Fedha leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo).

No comments:

Post a Comment