TANGAZO


Thursday, July 25, 2013

Rais Jakaya Kikwete anena: Hakuna wa kutuchezea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho kikwete, akiwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika leo, katika Kijiji cha Kaboya Wilaya ya Muleba, mkoani Bukoba. (Picha zote na Ramadhan Othman, Bukoba.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika leo, katika Kijiji cha Kaboya Wilaya ya Muleba, mkoani Bukoba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho kikwete, akiweka mkuki katika Mnara wa Mashujaa uliojengwa  katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika leo, katika Kijiji cha Kaboya Wilaya ya Muleba, mkoani Bukoba katika Siku ya maadhimisho ya Siku ya Mashujaa.
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya  Mashujaa walipozikwa katika kijiji cha Kaboya Wilaya ya Muleba mkoani Bukoba leo.
Kiongozi wa Mabalozi, balozi Juma Khafan Mpango, akiweka shada la mauwa katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wakati wa maadhimisho ya kuwaenzi na kuwakumbuka mashujaa hao, huko katika kijiji cha Kaboya Wilaya ya Muleba mkoani Bukoba.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba George Katando, akiweka upinde kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wakati wa maadhimisho ya kuwaenzi na kuwakumbuka mashujaa hao, huko katika kijiji cha Kaboya Wilaya ya Muleba mkoani Bukoba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongozwa na Mkuu wa Maeshi ya Ulinzi, Jenerali Devies Mwamunyange kutembelea makaburi ya mashujaa hao katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika Kijiji cha Kaboya Wilaya ya Muleba mkoani Bukoba.


*Asema ulinzi mipakani umeimarishwa
*Wasomi wasema JK ametuma salamu M23
Na Mwandishi Wetu, Kagera 
RAIS Jakaya Kikwete amesema mtu yoyote ambaye anataka kufanya chokochoko ya kutaka kuishambulia Tanzania hataachwa.
Amesema kuwa Serikali yake ipo makini katika kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa wakati wote huku akiweka wazi mipaka yote ya nchi kuwa ulinzi umeimarishwa vya kutosha.
Kauli ya Rais Kikwete inakuja wakati muafaka kwani tayari, baadhi ya nchi jirani zimeanza kutoa kauli za vitisho dhidi ya Tanzania ikiwemo nchi ya Rwanda ambayo imesema inaweza kufanya shambulio wakati sahihi ukifika.
Akizungumza leo mjini hapa wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa wa vita ya Uganda, Rais Kikwete alitumia nafasi hiyo kulihakikishia Taifa kuwa lipo salama na hakuna anayeweza kuthubutu kushambulia au kumega ardhi ya mipaka yetu.
"Hakuna mtu yeyote anayeweza kujitokeza na kutushambulia au anayeweza kujitokeza na kutaka kumega eneo la mipaka yetu.Hatutamuacha na kubwa zaidi mipaka yetu yote iko salama, ulinzi umeimarishwa,"alisema Rais Kikwete.
Akizungumzia zaidi usalama wa nchi akiwa katika Mkoa huo Kijiji cha Kaboya  ambako kuna makaburi wa mashujaa wa Tanzania waliopigana vita ya kumuondoa Idd Amin, Rais alisema ulinzi umeimarishwa kwenye mipaka yote.
"Mipaka yetu iko salama, ulinzi umeimarishwa na kila siku tunaendelea kuiimarisha.Hakuna anayeweza kutuchezea, "alisema Rais Kikwete.
Aliongeza wananchi wa Tanzania wanatakiwa kupuuza maneno ya mitaani na kusisitiza kuwa ulinzi wa kuwalinda kwa saa 24 upo wa kutosha na uwahakika.
Kauli ya Rais Kikwete pia inaonesha kutuma salamu kwa kundi la waasi wa M23 ambao siku za karibuni wametoa vitisho kuwa wanaweza kuishambulia Tanzania kutokana na kupeleka askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), kulinda amani Congo.
Katika maadhimisho ya mashujaa wa Tanzania , Rais Kikwete alisema anatambua umuhimu wa nchi kuwa salama, hivyo Serikali yake imejipanga vema katika kuhakikisha usalama unakuwepo wakati wote.
Kuhusu maadhimisho hayo Rais Kikwete alisema "mara nyingi maadhimisho haya tumekuwa tukiyafanya Dar es Salaam ,mwaka huu tumeamua kuyafanyia hapa kutokana na watu wengi walioathirika na vita hivyo kutokea Mkoa wa Kagera".
Alikumbusha pia , maadhimisho hayo yalishafanyika katika Mkoa wa Mtwara ambako pia kuna mashujaa waliozikwa katika mkoa huo kutokana na kushiriki mapambamano ya kuikomboa Msumbiji.
Akielezea cha
nzo cha vita vya Kagera ilivyotokea mwaka 1978, Rais Kikwete alisema ilitokana na uchokozi uliofanywa na aliyewahi kuwa Rais wa nchi ya Uganda  Iddy Amin kuivamia Tanzania kwa kumega sehemu ya ardhi kuanzia Mto Kagera kwa madai ipo karika ardhi ya Uganda.
"Baada ya kumega kipande hicho alikiuganiasha na ardhi ya Uganda na kisha kuipa jina la Wilaya ya Lakai, kitendo kilichopelekea Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Kwanza nchini, Hayati Baba wa Taifa Mwalimuj Julius Nyerere kuamuru jeshi kuondosha uvamizi huo.
Alisema kuwa baada ya kuikomboa ardhi iliyomegwa, pia jeshi lilifanya juhudi za pamoja kwa lengo la kumkamata  Iddy Amin lakini wakati jeshi likifanya hivyo aliweza kukimbia nchi yake na hakuweza kurudi mpaka umauti ulipomkuta akiwa nchi za Falme za Kiarabu.

Askofu Kilani
Akizungumza kabla ya Rais Kikwete, Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba, Method Kilaini alitumia nafasi hiyo kuwaombea viongozi ili waendele kuenzi amani nchini.
Pia alitaka viongozi wa Bara la Afrika  kuenzi amani na kuondosha machafuko yanyoendelea  Darfur,Kongo Kinshasa na sehemu zingine ulimwenguni ili wananchi wote waishi kwa amani.
Askofu Kilaini alimuomba Mungu ili aweze kueipusha Tazania isiingie kwenye uvunjifu wa amani kwani tayari kuna dalili ambazo zimeanza kujitokeza si nzuri akitolea mfano vitendo vya kurushwa mabomu kwenye mikutano ya hadhara kama ilivyotokea Arusha.
"Amani ihubiriwe kuanzia ngazi ya familia , makazini au katika vikundi mbali ambavyo wananchi wamekusanyika kwa lengo la kufanya mamabo yao ya kiuchumi" alisema Kilaini.

Mwamunyange
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Davis Mwamunyanye alisema kuwa wananchi hawana budi kulala usingizi na kuendelea na shughuli za uchumi kwani nchi iko katika mikono salama.

Katika maadhimisho hayo, pia viongozi wa ngazi mbalimbali Serikalini, walipata nafasi ya kushiriki pia walikuwepo wanasiasa wa vyama mbalimbali na viongozi wa dini zote.
Mbali ya Rais Kikwete kushiriki katika siku hiyo na kutoa hutuba kwa ajili ya Taifa hili, pia viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein walihudhuria sherehe hizo.
Pia viongozi wa dini zote nao walipata nafasi ya kuhudhuria na kutoa kauli mbalimbali zikiwemo za kulitakia taifa amani na mshikamano.
Akizungumza kabla ya Rais Kikwete, Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba ,Method Kilaini alitumia nafasi hiyo kuwaombea viongozi ili waendele kuenzi amani nchini.
Pia alitaka viongozi wa Bara la Afrika  kuenzi amani na kuondosha machafuko yanyoendelea  Darfur,Kongo Kinshasa na sehemu zingine ulimwenguni ili wananchi wote waishi kwa amani.
Askofu Kilaini alimuomba Mungu ili aweze kueipusha Tazania isiingie kwenye uvunjifu wa amani kwani tayari kuna dalili ambazo zimeanza kujitokeza si nzuri akitolea mfano vitendo vya kurushwa mabomu kwenye mikutano ya hadhara kama ilivyotokea Arusha.
"Amani ihubiriwe kuanzia ngazi ya familia , makazini au katika vikundi mbali ambavyo wananchi wamekusanyika kwa lengo la kufanya mamabo yao ya kiuchumi" alisema Kilaini.
Vongozi mbalimbali walishiriki katika maadhimisho hayo .Baadhi yao ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Ghalib Bilal,  Jaji Mkuu Othman Chande na Waziri wa Ulinzi Shamsh Vuai Nahodha.
Wengine ni Waziri wa Aridhi , Nyumba na Maendeleoa Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyege,Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Masawe na mbunge wa Kagera Mwijenga.
Kauli ya Rais Kikwete kuhusu usalama wa nchi, baadhi ya wasomi nchini walisema kuwa, kauli ya Rais ni salamu kwa kundi la waasi la M23 ambalo limetoa vitisho siku za karibuni lakini pia hata kwa viongozi wenye nia mbaya na Tanzania.

No comments:

Post a Comment