TANGAZO


Thursday, July 25, 2013

Wakala wa Vipimo (WMA) yaboresha mifumo ya ukaguzi

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa, akizungumza kabla ya kuwakaribisha baadhi ya viongozi wa Wakala wa Vipimo (WMA), kuzungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Meneja Sehemu ya Habari, Irene John na kulia ni Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege. (Picha zote na Kassim Mbarouk -www.bayana.blogspot.com)
Kaimu Meneja, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kazi na majukumu ya wakala pamoja na uboreshwaji wa mifumo ya ukaguzi. Kulia ni Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Kaimu Meneja, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kazi na majukumu ya wakala pamoja na uboreshwaji wa mifumo ya ukaguzi. Kulia ni Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Kaimu Meneja, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano huo leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kulia ni Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege na wapili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akizungumza na waandishi katika mkutano huo, Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kaimu Meneja Habari na Mawasiliano, Irene John na Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa. 
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akiwaonesha waandishi kipimo cha matenki ya mafuta wakati wa mkutano huo jijini leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kaimu Meneja Habari na Mawasiliano, Irene John na Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa. 
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akiwaonesha waandishi kifaa cha kutunzia kumbukumbu za upimaji wa magari kinachujulikana kwa jina la kitaalamu cha 'Scanner', wakati wa mkutano huo leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kaimu Meneja Habari na Mawasiliano, Irene John na Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na uongozi huo katika mkutano huo jijini leo.
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akiwaonesha waandishi wa habari namna wafanyabiashara wanavyowapunja wanunuzi wa bidhaa kwa njia ya vipimo vya mizani, wakati taasisi ya Wala wa Vipimo (WMA), walipokuwa wakizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu kazi na majukumu ya wakala hiyo pamoja na uboreshawaji wa mifumo ya ukaguzi. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kaimu Meneja Sehemu ya Habari, Irene John na Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa. 
Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno (kushoto), akifafanua jambo katika mkutano huo leo.
Kaimu Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo Tanzania Irene John akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia wakala hao kuboresha mifumo ya ukaguzi. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari,  Zamaradi Kawawa. (Picha na Elphace Marwa) 
Meneja Vipimo toka Wakala wa Vipimo Tanzania Deogratius Kadeghe akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya jiwe halisi linalotakiwa kutumika kwa ajili ya vipimo vya bidhaa mbalimbali, katika mkutano uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.  (Picha na Elphace Marwa)


Wakala wa Vipimo ni mojawapo ya Wakala za Serikali ambayo ilianzishwa  tarehe 13  Mei, 2002 kwa Tangazo la  Serikali namba 194 la tarehe 17 Mei, 2002. Lengo la Serikali kuanzia wakala wa Vipimo ilikuwa ni  kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Awali, ilikuwa ni Idara ya Serikali chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Ø  Jukumu  kuu la Wakala wa Vipimo  ni kumlinda mlaji  kupitia matumizi ya vipimo sahihi.
Pamoja na huduma zake nyingi  inazotoa Wakala wa Vipimo, kwa leo tutaueleza umma wa watanzania kuwa tumeboresha  mfumo wa ukaguzi  wa  bidhaa zilizofungashwa. Mfumo huu wa sasa ni wa ki-electronic ambao umeongeza ufanisi na  kurahisisha kazi za ukaguzi tofauti na hapo awali ambapo tulikuwa tukitumia njia ya kupima na kukokotoa  kwa calculator njia  ambayo ilikuwa ikichukua muda mrefu  siku mbili  au zaidi  hadi kutoa uamuzi.
 Faida za kutumia mfumo mpya katika bidhaa zilizofungashwa;
a.    Unarahisisha kazi (simplify work) eg. zamani tulikuwa tunatumia siku 2 hadi 3 katika ukaguzi wa bidhaa ya aina  moja  kwa sasa nusu saa  inatosha  kukamilisha kazi hiyo.
b.    Utendajika kazi unakuwa wa uhakika na  ni wa wazi (measurement results are more accurate and reliable).
c.    Mteja anaona kazi iliyofanyika ni ya ufanisi,  ya kitaalamu  na anapata matokeo ya haraka hivyo anaridhika  na huduma anayopatiwa (customer satisfaction).
d.    Mteja anakuwa tayari kulipa ada (create willingness of customers to pay for service rendered)

Pia, wakala wa Vipimo  imeboresha ukaguzi wa  malori yabebayo  mafuta (Road Tankers)  pamoja na malori yabebayo mchanga na kokoto,( Sand and Other Ballast Lories (SBLs) kwa kutumia  Kifaa maalum  kinachojulikana kama scanner tofauti na hapo awali tulipokuwa tukikagua  kwa kuangalia nyaraka ( certificates)   kwa macho.   Kwa upande wa   Malori yabebayo  mafuta tulikuwa tukiangalia chart pamoja na  Dip stick  Utaratibu huo ulikuwa  ni rahisi kugushiwa na malori ya mchanga tuliwa tukichora ubavuni kuonesha  ujazo wa  lori husika.

Njia ya sasa ya kutumia scanner ;
a.    Utendaji kazi wake unakuwa ni wa uhakika na sahihi zaidi katika kubaini sticker halisi kwa magari yaliyokaguliwa. Hii inatupa uhakika kuwa gari limepimwa  kwa mwaka husika.
b.    Kupunguza au kuondoa udanganyifu kwa wamiliki wa malori  hayo.
c.    Mteja kulidhika na ukaguzi huo.

Faida ya Mifumo  kwa Serikali: Itasaidia nchi ya Tanzania kufanya biashara nje ya nchi sababu taratibu za ufungashaji zitakuwa zimezingatiwa hasa uhakiki wa vipimo.

Faida ya Mifumo kwa Wananchi: Wananchi kama walaji wa mwisho  wanahakikishiwa usahihi  wa vipimo kwa bidhaa watakazolipia.  

Wito kwa watanzania;  Tusaidiane kutoa taarifa pale mnapohisi au kuona wafanyabiashara wasiowaaminifu wanatumia vipimo pungufu au batili kwa kuwasiliana na ofisi zetu zinazopatikana kila mkoa.

 Asanteni kwa kunisikiliza

No comments:

Post a Comment