TANGAZO


Tuesday, June 18, 2013

Waziri wa Utumishi, Celina Kombani ahutubia mkutano wa Siku ya Utumishi nchini Ghana

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Mawaziri wa Utumishi wa Umma barani Afrika, Celina Kombani (MB), akihutubia katika sherehe za ufunguzi wa Siku ya Utumishi wa Umma barani Afrika, nchini Accra Ghana leo.
Baadhi ya waalikwa kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani (MB), wakati alipokuwa  akihutubia katika mkutano huo, ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, George Yambesi, wakiwa katika banda la Tanzania pamoja na baadhi ya watumishi wengine wa ofisi yake, mara baada ya kuhutubia kutano huo. 
Waziri Kombani (MB), akitoa maelekezo kwa baadhi ya washiriki wa Tanzania kwenye banda hilo. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi.

Washiriki wengine kutoka Tanzania wakipewa maelekezo na Waziri Kombani (MB), Kombani. (Picha zote kwa hisani ya Ofisi ya Rais -Utumishi wa Umma)

No comments:

Post a Comment