Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, wakibadilishana hati za makubaliano ya mkopo wa riba nafuu, mjini Dodoma leo. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa akizungumza na waandishi wa habari, mjini Daodoma leo kuhusu mkopo wa riba nafuu wa shilingi bilioni 77.7, utakaotolewa na Japan kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es Salaam na fedha nyingine kutumika kwa ajili ya kupunguza umaskini nchini. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na kulia ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada.
Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, akizungumza katika hafla hiyo, mjini Dodoma leo mara baada ya kusaini na Tanzania hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu, ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA, jijini Dar es Salaam na fedha nyingine kusaidia katika kupunguza umaskini. Katikati ni Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa na kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) nchini, Yasunori Onishi, akizungumza katika hafla hiyo, mjini Dodoma leo.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (katikati) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan nchini (JICA), Yasunori Onishi (kulia), wakijiandaa kusaini hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA, jijini Dar es Salaam na fedha nyingine kutumika kwa ajili ya kusaidia kupunguza umaskini nchini. Hafla hiyo imefanyika leo, mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (katikati) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan nchini (JICA), Yasunori Onishi (kulia), wakisaini hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA, jijini Dar es Salaam na fedha nyingine kutumika kusaidia kupunguza umaskini nchini. Hafla hiyo imefanyika leo, mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan hapa nchini (JICA), Yasunori Onishi (kulia) na Waziri wa Fedha wakibadilishana hati ya mkopo wa fedha za ujenzi wa daraja la juu katika makutano ya TAZARA, mjini Dodoma leo, mara baada ya kuweka saini hati hizo, ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi huo. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okada na wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo, mjini Dodoma kuhusu juhudi za Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam, mara baada ya Tanzania na Japan kusaini makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 52.5 kutoka Japan kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara za Juu katika makutano ya TAZARA.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo, mjini Dodoma katika hafla hiyo. (Picha zote na mpigapicha wetu)
No comments:
Post a Comment