TANGAZO


Tuesday, June 18, 2013

Vodacom yapanua wigo huduma na ajira kwa Watanzania


Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Upendo Richard (kulia), akimkabidhi funguo  Meneja wa duka jipya la Vodacom, lililopo kwenye jengo la Millennium Tower, ghorofa ya kwanza, Miriam Minja, wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano cha Kampuni hiyo, Joseline Kamuhanda.


Meneja wa duka jipya la Vodacom lililopo kwenye jengo la Millennium Tower, ghorofa ya kwanza, Miriam Minja, akifungua duka hilo, kwa mara ya kwanza, tayari kwa kutoa huduma kwa wateja wa Kampuni hiyo, akishuhudiwa na Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Upendo Richard (kulia) na Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Joseline Kamuhanda.
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda, akiongea na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo, lililopo kwenye jengo la Millennium Tower, ghorofa ya kwanza. Duka hilo linaanza kutoa huduma rasmi leo, kwa wateja wake.
Meneja wa duka jipya la Vodacom lililopo kwenye jengo la Millennium Tower, ghorofa ya kwanza, Dar es Salaam, Miriam Minja, akimuonesha hali ya umbo na utendaji kazi wa moja ya simu zilizokuwemo kwenye duka hilo, mteja Lameck Hanold, alipotembelea duka hilo, wakati wa uzinduzi wake leo. Kushoto anayeangalia ni Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Upendo Richard. 

• Watanzania zaidi kuendelea kupata huduma za mawasiliano
Dar Es Salaam, June 18, 2013
HUKU jiji la Dar es Salaam likiendelea kukua kwa kasi na kushuhudia ongezeko kubwa la watu kutoka sehemu mbalimbali, upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii umekuwa ukikabiliwa na changamoto kadhaa kutokana na kasi ya utoaji huduma kutoendana na kasi ya ongezeko la watu.

Katika kukidhi haja hiyo, ya utoaji wa huduma kwa wateja na elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeendelea kupanua wigo wa ajira na huduma kwa kufungua duka la huduma kwa wateja katika jengo la Milenium Tower, lililoko Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia wakati wa uzinduzi wa duka hilo leo, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda, amesema Vodacom ni kampuni pekee ambayo imeendelea kuongoza kwa kuwa na maduka mengi ya mauzo na huduma kwa wateja kwa kufikisha maduka 66 ikiwa ni kampuni pekee kuwa na maduka mengi ya huduma na kufanikisha adhma ya kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo, huku Dar es Salaam ikiwa na idadi ya maduka 21.

“Ukuaji wa huduma kwa kampuni ya Vodacom umekuwa kwa kasi, huduma kama ya M – Pesa sasa imepanuka kwa kasi na kutoa huduma kwa watanzania zaidi ya milioni 10. Kufuatia mafaanikio haya tunalazimika kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa wateja  ni wa uhakika” alisema Kamuhanda.

“Kuongoza katika sekta ya mawasilaino kuna changamoto zake, lazima tuhakikishe tunaendana na kasi ya ukuaji na ongezeko la watu na uhitaji wa huduma zetu kwa watu wa aina mbalimbali.

Aidha Kamuhanda alisema kuwa Kufunguliwa kwa duka hilo sasa sio tu kunaboresha upatikanaji wa huduma pia ni fursa pekee ya kuendelea kupanua wigo wa ajira kwa watanzania.

“Ufunguzi wa duka hili unatoa fursa ya ajira kwa watanzania, ambapo wafanyakazi wapatao 3 watatoa huduma kwa wateja wetu hivyo ni hatua kubwa kwa kutengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya. Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 450,000 wenye ajira zisizo rasmi,” alisema Kamuhanda.

No comments:

Post a Comment