TANGAZO


Wednesday, June 5, 2013

Vodacom yalipa Sh.36 bn, kodi ya mwaka



  • Zaidi ya Bilioni 200 zawekezwa kuboresha mtandao.
Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mawasiliano ya 

Vodacom Tanzania imetangaza 

kuchangia jumla ya Sh36.6 

bilioni (Tsh36,509,063,334/-) 

kama malipo kodi ya kampuni 

kwa mwaka wa fedha wa 2012/ 

2013. 

Huku Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza 

akibainisha kuwa malipo hayo ni ongezeko la zaidi ya mara 20 

ya kile kilicholipwa na kampuni hiyo kwa miaka mitatu iliyopita.


Mkurugenzi Meza, akitoa ufafanuzi huo juzi, alisema kuwa kampuni hiyo, imefanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha mtandao na huduma  kwa miaka kadhaa iliyopita na sasa malipo hayo ni sehemu ya mavuno ya uwekezaji huo ambao pia umekuwa na mchango mkubwa kwa kuchangia katika pato la taifa.

Kodi nyingine zilizolipwa na kampuni hiyo kwa ujumla kwa mwaka 2012 ni kiasi cha Sh190.7 milioni (Tsh190,754,776,956/-). Kiasi hicho kimegawanyika katika makundi yafuatayo, Sh. 4,565,183,461/- kama kodi ya zuio, Sh. 92,322,077,623/- kama kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Sh 51,337,344,600/- kama Ushuru wa bidhaa, Sh. 4,530,171,272/- katika Ada ya Udhibiti, na 2,576,227,649/- kama mchango wa mfuko wa huduma za mawasiliano (Universal Communications Services Access Fund ) kwa mwaka 2012.

Malipo mengine ya Kodi na Ushuru yanafikia jumla ya Shilingi bilioni 34/- katika majumuisho ya malipo ya mwaka huu wa fedha ikijumuisha Ada ya Ushuru na forodha, Kodi ya Mapato.

Meza amesema kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2012/13, kampuni yake iliwekeza zaidi ya bilioni 200/- katika kuboresha mtandao na huduma. 

Uwekezaji ambao umeiwezesha kampuni kuongeza maradufu uwezo wa mtandao wake hadi kufikia mwezi machi 2013. Uwekezaji huo umefikisha kiasi cha shilingi trilioni 1.3 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.

Aidha, Meza ameongeza kuwa Kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za uhakika za mawasiliano kokote nchini, huku akisisitiza kuwa kwa kampuni yake kuendelea kuwekeza katika mtandao wa 3G pamoja na kujiunga katika mkongo wa taifa wa mawasiliano ni ishara tosha ya jitihada zake.

Pamoja na mambo mengine Vodacom iliwekeza kiasi cha Shilingi bilioni 800 katika mradi wa kujiunga na Mkongo wa mawasiliano wa taifa baada ya kujiunga na mkongo huo kwa kanda ya kaskazini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Dodoma.

“Kujiunga katika mkongo wa Taifa wa mawasiliano pamoja na uwekezaji katika mtandao wa 3G kumewawezesha wateja wetu kupata huduma za intaneti kwa kasi zaidi tofauti na ilivyokuwa awali, Haya ni mafanikio makubwa katika sekta ya mawasiliano, Uwekezaji huu umechangia na kuwawezesha watanzania kuchangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” alisema Meza.

Aliongeza kuwa, “sasa tunafanya jitihada katika kuunganisha kanda ya Magharibi itakayo unganisha mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Singida, Kigoma na Makambako, na Kanda ya Kusini itakayo jumuisha mikoa ya Morogoro, Coast, Iringa, Ruvuma, Mtwara, Lindi and Dar es Salaam katika kuunganishwa na mongo wa taifa wa mawasiliano.


Katika kuboresha huduma za mawasiliano ya kisasa na teknolojia ya hali ya juu nchini mwaka uliopita, Vodacom ilizindua matumizi ya teknolojia ya hali ya juu zaidi duniani ya LTE Msasani Peninsula jijiji Dar es Salaam, teknolojia hii ambayo pia inajulikana kama 4G inawawezesha watumiaji kupata internet yenye kasi ya juu zaidi kuliko yoyote ili nchini.

Meza amebainisha kuwa Vodacom inajivunia mafanikio kwa kazi kubwa ambayo imefanya katika kuboresha huduma za jamii (CSR). 

Kwa mwaka 2012 kampuni hiyo kupitia kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom Foundation kimetumia zaidi ya Shilingi bilioni 9.6 katika sekta ya Afya, Elimu na Uwezeshwaji wa Kiuchumi kwa wananchi kupitia miradi mbalimbali nchini.

Vodacom Foundation imefadhili zaidi ya miradi 120, ikiwa katika sekta mbalimbali ukiwemo mradi wa kuondoa Fistula nchini Tanzania, Utoaji wa vifaa vya ujenzi na mafunzo mashuleni, uwezeshwaji wa kiuchumi kwa wanawake katika maeneo ya vijijini pamoja na miradi ya maji katika maeneo yenye usumbufu wa huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment