Spika wa Bunge, Anne Makinda akitoa ufafanuzi wa hali iliyotokea bungeni leo, mjini Dodoma wakati wa kikao cha Bunge. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akiongea na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika katika Viwanja vya Bunge leo, baada ya hoja yake binafsi kukataliwa bungeni.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela akiongea na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja katika viwanja vya Bunge, mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo (kushoto) pamoja na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi, wakiwa katika kikao cha Bunge, wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa bungeni, mjini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia (kushoto), akimsikiliza Mhandisi Stella Manyanya (Viti maalumu), kuhusu yaliojiri Bungeni leo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdalla Kigoda (kulia), akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid katika viwanja vya Bunge, mjini Dodoma leo baada ya kikao cha bunge kuahirishwa.
No comments:
Post a Comment