TANGAZO


Wednesday, June 5, 2013

Kenya: 0 Nigeria: 0 baada ya dakika 45



Nigeria wanasemekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda mechi ya leo
Mchuano wa kufa na kupona unashuhudiwa kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani mjini Nairobi.
Imepita dakika 44 tangu kuanza kwa mechi na bado wote wako sare tasa yaani bila bila.
Hii ni mechi ya mkondo wa pili kwa timu hizo mbili baada ya kwenda sare ya bao moja kwa moja walipocheza kwa mkondo wa kwanza mjini Calabar Nigeria mwezi jana.
Mechi hii ni ya kundi la F ya kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Vijana wa kocha Stephen Keshi, wanatarajiwa kuendeleza ushindi wao hii leo wakijitafutia nafasi ya kuwakilisha Afrika katika michauno ya kombe la dunia nchini Brazil
Kwa vijana wa Eagles wanaosemekana kujiandaa vyema, wanafahamu kuwa ikiwa watashindwa basi itakuwa hasara kwao kwani hawataweza kwenda Brazil.
Licha ya kwenda sare mwezi jana, Nigeria inaingia kwenye mkondo huu bila ya kushindwa mechi yoyote ya makundi kati ya kumi na sita zilizocheza hadi kufikia sasa.
Wadadisi wanasema Eagles wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda. Mwandishi wetu Odeo Sirari amepiga kambi katika uwanja wa Moi Kasarani kutupasha habari. Na wewe shabiki una fursa ya kutupasha yanayojiri huko pia kupitia kwa ukurasa wtu wa BofyafacebookBofyabbcswahili

14:50 PM :Shamra shamra zimeanza kupamba moto katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani. Mwandishi wa BBC ambaye yuko katika uwanja huo Odeo Sirari, anasema kuw mashabiki wanzidi kumiminika uwanjani. Milango ya uwanja ilifunguliwa rasmi majira ya saa tano asubuhi
14:58 PM: Mojawapo ya mabango ya mashabiki uwanjani yana bendera ya Kenya na maandishi ''Oga you are finished'' kwa maana kuwa Nigeria itashindwa . Odeo anasema hayo ni maoni ya mashabiki wa Nigeria uwanjani

Timu zote zina mbili zina uhakika zitashinda mechi ya leo. Tuache tuone msema kweli
Mechi inatarajiwa kuanza saa kumi kamili. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria

15:43 PM: Mashabiki washangilia wachezaji wa Harambe Starrs wakiingia uwanjani. Super Eagles nao pia wameingia uwanjani . Wachezaji wa pande zote mbili sasa wanapasha misuli joto
15:48 PM: Uwanja wa michezo wa Moi Kasarani una uwezo wa kushenei mashabiki takriban 60,000

15:49 PM: Kikosi cha Harambe Stars: Mlinda lango Duncan Ocheng, Safu ya ulinzi David Owino Brian Mandela David Ochieng . Wachezaji wa kiungo cha kati Mulinge Ndeto, Victor Wanyama Jamal Mohammed,Johana Omolo na Peter Opiyo. Washambulizi ni Kefa Aswani na Fracis Kahata
16:07 PM: Mechi imeng'oa nanga rasmi . Kikosi cha Eagles...Efe, Oboabona, Omeroo Elderson, Onazi, Mikel, Mba,Oduamadi,Musa, Ideye Golikipa ni Enyeama

16:33 PM baada ya mechi kuchezwa kwa zaidi ya dakika thelathini bado timu hizo ziko sare tasa
16:39 PM Humphrey W. Musungu kupitia ukurasa wetu wa Bofyafacebookanasema David owino ajeruhiwa lakini anashughulikiwa
16:41 Mshambuliaji wa Kenya Kepha Aswani anenekana akichechema uwanjani na kuwa mashabiki wanataka aondolewe

16:51 shambulizi katika eneo la hatari lango la timu ya Kenya. Sunday Mba aliupiga mpira kwa kichwa lakini ukapaa juu ya mlingoti wa goli . Mashabiki wa Kenya wabaki kimya.

No comments:

Post a Comment