TANGAZO


Tuesday, June 4, 2013

Tigo yasaidia Mpango wa Taifa wa Damu Salama shilingi mil. 30

Ofisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya  simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati kampuni hiyo, ilipokabidhi msaada wa shilingi milioni 30 kwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Efespo Nkya. (Picha zote na Kassim Mbarouk wa bayana.blogspot)
Mkurugenzi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Efespo Nkya, akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Ofisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakisikiliza na kunukuu maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika hafla ya kukabidhi msaada huo.
Waandishi wa habari, wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika hafla ya kukabidhi msaada huo.
Ofisa Mahusiano ya Jamii na Matukio wa Kampuni ya  simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael,  akiwakabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 30,  Mkurugenzi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Efespo Nkya (kushoto) na Ofisa Masoko na Mahusiano wa mpango huo, Rayah Hamad, zilizotolewa na kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Efespo Nkya na Ofisa Masoko na Mahusiano wa mpango huo, Rayah Hamad, wakinyanyua mfano wa hundi ya Shilingi milioni 30, zilizotolewa msaada kwa mpango huo na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment