Msaidizi wa rais wa Misri ameomba radhi kwa kukosa kuonya wanasiasa kuwa mapendekezo yao kuhusu jinsi ya kuizuia Ethiopia kujenga bwawa katika mto Nile,ikiwemo kuchukua hatua za kijeshi yalikuwa, yalikuwa yakipeperushwa moja kwa moja kupitia televisheni.
Msaidizi huyo Bakinam al-Sharqawi, aliomba radhi kwa aibu yoyote waliyopata viongozi hao ambayo huenda ilitokana na kitendo hicho.
Matamshi hayo yalitolewa Jumatatu wakati wa mkutano na Rais Mohammed Morsi. Mependekezo yaliyotolewa ni pamoja na kutumia nguvu za kijeshi kuharibu bwawa hilo pamoja na hata kuunga mkono makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya serikali ya Ethiopia.
Rais Mnorsi aliitisha mkutano huo kutathmini athari za ujenzi wa bwawa la Ethiopia katika sehemu ya maji ya mto Nile yanayomilikiwa na Misri.
Washiriki wa mkutano huo hawakujua kuwa walikuwa wanatizamwa kwenye runinga wakati wakitoa matamshi yao bila ya kujali.
Mapendekezo yao yalikuwa pamoja na kuonya Ethiopia kuwa inatutumia nguvu za kijeshi dhidi yake ikiwa itaendelea na mpango wake wa ujenzi wa Bwawa kwenye mto Blue Nile.
Moja wa wanasiasa, alipendekeza kutuma kikosi maalum kuharibu bwawa hilo, mwingine akisema kuwa watatuma ndege za kivita kutisha Ethiopia wakati wa tatu akisema kuwa wangeunga mkono waasi wanaopambana na serikali ya Ethiopia.
Misri ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu Mashariki ya Kati na hutegemea sana maji ya mto Nile ambao ndio mto mrefu zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment