Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kulia akikaribishwa kwa ngoma ya Ndege mara alipowasili katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kulia akiangalia Ngoma inayochezwa na Watoto mara alipowasili katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.
Rais wa Zaanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akiangalia mchezo wa Bao la kete baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.kulia yake ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na kushoto yake ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo Mwinyi Jamal Ramadhan.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akiangalia Picha zilizochorwa kwa Ustadi pamoja na mazulia katika moja ya mabanda yaliokuwepo katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akichangia Upatu wa Maridadi ambao hutolewa baada ya Mwana kuolewa na watu kunywa chai(Kombela Bwana Harusi) katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba ya makaribisho katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.kushoto yake ni Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akisalimiana na Mzee Issa Suleiman Issa katika nyumba ya kiasili iliojengwa kwa makuti ya Kumba ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Tamasha la Urithi la watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini "B"Unguja. (Picha zote na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar)
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza matumaini yake kuwa Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Watu wa Mangapwani litatoa fursa ya kukitangaza kijiji hicho kwa watalii wa ndani na nje ya nchi sambamba na kuuimarisha utamaduni, mila na desturi ya Mzanzibari.
Dk. Shein alisema kuwa Magwapwani inasifika ulimwenguni kwa taswira njema na ufukwe wa bahari wenye ngome za majabali yaliyozungukwa na mchanga mweupe pepepe na laini.
Hayo aliyasema leo katika ufunguzi wa Tamasha la Urithi wa Mila na Utamaduni wa Watu wa Mangapwani, uliofanyika huko Magapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja, na kusisitiza kuwa kuwa Magwapwani inasifika ulimwenguni kwa taswira njema na ufukwe wa bahari wenye ngome za majabali yaliyozungukwa na mchanga mweupe pepepe na laini.
Dk. Shein alisema kuwa matamasha ya aina hiyo yana umuhimu mkubwa nchini na kueleza kuvutiwa kwake na ubunifu wa kuandaa tamasha hilo ambalo linajumuisha shughuli mbali mbali za sanaa, michezo ya asili na harakati nyengine ambazo ni kielelezo cha utamaduni wa watu wa Mangapwani na Zanzibar kwa ujumla.
Alisema kuwa matamasha kama hayo huwaonesha na kuwafundisha wageni na watalii wanaoitembelea Zanzibar namna ya utamaduni wa Kizanzibari na kutoa wito kwa vijana kuuendeleza utamaduni wao na kuona fahari kuutangaza ndani na nje ya nchi.
Aidha, alisisitiza haja kwa matamasha kama hayo yakatumika kukuza umaarufu wa wasanii wakongwe kama Marehemu Bibi Siti binti Sadad, Marehemu Bi Fatma binti Baraka (Bi Kidude) na Marehemu Bwana Bakari Abeid na kuzieneza kazi zao kwa kadri inavyowezekana.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye ni mlezi wa Tamasha hilo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuutunza na kuuendeleza utamaduni wa asili kuanzia lugha ya Kiswahili mpaka Tamasha kama hilo la utamaduni.
“Tamasha hili limefanyika katika wakati mzuri na kwenye eneo linalostahiki, yaani eneo la Mangapwani eneo hili linahistoria kubwa inayojulikana katika sehemu mbali mbali kutokana na matukio kadhaa pamoja na uzuri wake wa kimaumbile”,alisema Dk. Shein.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza kufarajika kwake kutokana na tamasha hilo kutoa msukumo na ukumbusho wa shughuli mbali mbali za ibada ikiwemo dhikiri na kueleza kuwa kufana kwa tamasha hilo kunaonesha wazi kuwa watu wa Mangapwani wanaendelea kuishi kwa kusikilizana, kupendana, na wana mshikamano na umoja miongoni wmao.
Kutokana na mafanikio hayo, Dk. Shein alitoa nasaha zake kwa wananchi wa Mangwapwani kudumisha umoja walionao ili waendelee kufanya mambo makubwa zaidi kwa maslahi ya kijiji chao na nchi nzima kwa jumla.
Dk. Shein alieleza haja ya kuandaliwa kitabu maelezo yaliyotolewa na Mzee Ali Hassan Mwinyi juu ya historia ya kijiji hicho ili yaonekanwe na kufundishwa na kusisitiza haja ya kufanyika kila mwaka kwa maonyesho hayo.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kuifanya sekta ya utalii kuwa ni sekta mama katika kuinua uchumi ambapo dhamira hiyo imekuwa ikitekelezwa chini ya dhana ya ‘utalii kwa wote’.
Dk. Shein alipokewa kwa ngoma ya ndege na kualiaangalia maonyesho ya vitu mbali mbali yakiwemo mchozo wa bao, kutangwa, ngoma ya msewe aliyochezwa na watoto, harusi ya kizamani pamoja na shughuli zinazofanywa na watu wa Mangapwani na maonesho mengineyo ya vitu kadhaa yakiwemo majaribio ya sayansi yaliyooneshwa na wanafunzi
Mapema Mwenyekiti wa Tamasha hilo Mwinyi Jamali Ramadhani alieleza kuwa lengo kubwa la Tamasha hilo ni kuonesha utamaduni, silka na desturi za kale za watu wa Magapwani ambazo ziliachwa kwa muda mrefu.
Aidha, Mwenyekiti huyo alieleza azma ya Wanamangapwani ya kujenga chuo cha kufundisha masuala ya uvuvi wa kisasa, kutoa mafunzo ya uzamiaji na mafunzo mengine ya ufundi na kuiomba serikali kupatiwa eneo la ujenzi wa chuo hicho ambapo ombi hilo lilikubaliwa na Rais kwa kulifikisha kwa Wizara husika.
Nae Mlezi wa Tamasha hilo Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alieleza historia ya kijiji hicho cha Mangapwani tokea wakati wa ukoloni na kusisitiza kuwa eneo hilo lina utajiri mkubwa wa vivutio vya kitalii ambavyo vikitumika vizuri vitaimarisha uchumi wan chi.
Alisema kuwa sehemu hiyo ilikuwa na utamaduni wa Kizanzibari ikiwemo taarabu na kutunga njyimbo zilizotoa mafunzo, zilizostarehesha na kukuza Kiswahili.
Aidha, alieleza kuwa huo ni mwanzo mzuri kwa kijiji hicho na kueleza kuwa ipo haja kwa vijiji vyengine kufufua tamaduni, silka na desturi zao. Tamasha hilo limejumuisha maonyesho ya mapishi ya vyakula vya asili kama ugari wa muhogo na vyengine.
Eneo ambalo linahusishwa na biashara ya utumwa katika miaka ya 1840 hadi 1880 pia, ilikuwa ni tegemeo kubwa katika kulinda kisiwa cha Unguja wakati wa Vita vya Pili vya Dunia kwenye miaka ya 1939 hadi 1945, ambapo ngome zilizotumika zimebaki na kuwa kivutio kwa watalii kutoka pande zote za dunia.
No comments:
Post a Comment