TANGAZO


Friday, June 14, 2013

Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika, Waziri Sophia Simba, azungumza na waandishi wa habari, azindua Mtandao wa Mawasiliano wa kumlinda mtoto

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, yatakayofanyika kimikoa nchini kote Juni 16, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Famila kutoka wizara hiyo, Rose Minja na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Watoto, Benedict Missani. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, yatakayofanyika kimikoa nchini kote, Juni 16, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Watoto, Benedict Missani na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Vicent Tiganya.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Famila kutoka wizara hiyo, Rose Minja na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Watoto, Benedict Missani.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Sophia Simba, wakati alipokuwa akizungumza nao kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Dar es Salaam leo. Maadhimisho hayo yatafanyika Kimikoa nchini kote, Juni 16, mwaka huu.


Na Joseph Kanyopa, DSJ
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ametoa fursa kwa watoto kujieleza, kusikilizwa, kushiriki na kuonyesha vipaji vyoa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri huyo alisema kuwa kila mwaka tarehe 16 juni nchi 51 za umoja wa Afrika hadhimisha siku ya mtoto wa afrika kutokana na mauaji ya kikatili yaliyotokea nchini afrika tarehe 16 juni ambapo watoto wapatao 2000 wliuwawa kikatili na serikali ya kikaburu wakiwa katika harakati za kudai haki yao ya msingi ya kuto kubaguliwa kutokana na rangi yao.

Aliendelea kusema kuwa  Tanzani ni nchi mojawapo iliyo kwenye umoja wa nchi za Afrika ambapo kwa mwaka huu inatimia miaka 22 mfululizo tangu mwaka1991 katika kuadhimisha siku hiyo ya mtoto wa Afrika 

Hataivyo, Waziri alisema kuwa lengo na madhumuni ya maadhimisho haya kwa mwaka huu ni kuelimisha watu kuhusu haki,ustawi na maendeleo ya watoto wa jinsia zote,Pia watoto watapewa nafsi ya kujiereza ,kusikilizwa na kuonyesha vipaji nyao katika hatua za kujiendeleza wakati wa maadhimisho hayo

"Madhumuni ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika ni pamoja na kuinua kiwango cha uelewa na ufahamu wa matatizo yanayowakabili watoto wa Afrika"alisema 

Akitoa maelezo ya kina Sophia alisema kuwa upo umuhimu wa kuwakumbusha watu kuhusu uwelewa na ufahamu wa matatizo ya watoto kwani watu wengi hawafahamu matatizo ya watoto kitu kinachopelekea ongezeko la watoto wa mitaani 

Vilevile aliendelea kusema kuwa mbali na kutoa uwelewa  na ufahamu kwa watu pia Serikali ina lengo la kukumbusha na  kuhamasisha jamii kuhusu utoaji wa haki za msingi za watoto,kuhimiza kuweka rasilimali za kutosha katika afya,elimu na lishe bora ya watoto kama haki zao za msingi,katika maadhimisho hayo

Aliendelea kusema kuwa kila mwaka katika maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika Taifa huadhimisha siku hiyo kwa kuwa na kauli mbiu ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni 'Kuondoa mila zenye kuleta madhara kwa watoto ni jukumu letu sote'

Alimalizia kwa kusema kwa mwaka huu madhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yatafanyika katika ngazi ya mikoa ambapo kila mkoa utaadhimisha siku hii kwa kushilikiana na Halimashauri ya wilaya,manispaa,miji,kata na vijiji hii itaipa mikoa nafasi nzuri ya kutafakari matatizo yanayowakabili watoto ikiwa ni pamoja na kuwapatia haki zao za msingi na pia itapata nafasi ya kuweka miradi endelevu kwa ajili ya kuwaendeleza watoto.



Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kibasili wakiwa katika uzinduzi wa Mtandao wa Mawasiliano ya simu wa C-Sema, Piga 116 kwa ajili ya kumlinda mtoto, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akizungumza, wakati alipokuwa akizindua mtandao wa mawasiliano ya simu wa C-Sema, Piga 116, kwa ajili ya kumlinda mtoto jijini leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi huo, wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, alipokuwa akizungumza.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kibasili wakiwa katika uzinduzi wa Mtandao wa Mawasiliano ya simu wa C-Sema, Piga 116 kwa ajili ya kumlinda mtoto, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Maofisa wa C-Sema, ambao ndio wanaousimamia mtandao huo, kwa ajili ya kuwalida watoto, wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mtandao huo.
Baadhi ya Maofisa na wawakilishi wa taasisi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akizungumza, wakati wa uzinduzi wa mtandao wa mawasiliano ya simu wa C-Sema, Piga 116, kwa ajili ya kumlinda mtoto jijini leo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akiongea na simu, wakati alipokuwa akizindua mtandao wa mawasiliano ya simu wa C-Sema, Piga 116, kwa ajili ya kumlinda mtoto, Dar es Salaam leo. Wengine, waliomzunguka ni watoto kutoka Shule ya Msingi ya Buza na Sekondari ya Kibasila.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akibonyeza kitufe cha simu, wakati alipokuwa akizindua mtandao wa mawasiliano ya simu wa C-Sema kwa ajili ya kumlinda mtoto, Dar es Salaam leo. Wengine, waliomzunguka ni watoto kutoka Shule ya Msingi ya Buza na Sekondari ya Kibasila.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akiwa pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Buza na Sekondari ya Kibasila, mara baada ya kuzindua mtandao huo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akiwa pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Buza na Sekondari ya Kibasila, mara baada ya kuzindua mtandao huo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali zilikuwepo katika uzinduzi huo.

Na Nyendo Mohamed
WANANCHI wametakiwa kutumia vyema Mtandao wa Mawasiliano ya Simu  wa Kusaidia Watoto kwa kutoa taarifa zenye ukweli zinazohusu vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa.

Hayo aliyasema Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto, Sophia Simba leo, alipokuwa akizindua Mtandao wa Mawasiliano ya Simu wa Kusaidia Watoto utakaowasaidia watoto na jamii kwa ujumla kutoa taarifa zinazohisu ukatili wa kunjisia kwa watoto kwa kupiga namba 116.

Alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na utafiti uliofanywa na Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia na watoto mwaka 2009 ambayo imeonesha kuwa suala la ukatili kwa watoto kijinsia, kiakili na kimwili ni mkubwa mno. 

Simba alisema kuwa mtandao huu utasaidia kwa kiwango kikubwa kwa watoto na wakinamama pamoja na wanachi kwa ujumla kutokuwa na uoga wa kutoa taarifa hizo za kikatili.

Aliongeza kuwa wananchi wanatakiwa kutumia mtandao huo vyema ni kwa kutoa taarifa za ukweli ili kuwafanya watoto kupata huduma hizo.

Hata hivyo alisema kuwa mtanado huo utaanza kufanya kazi katika wilaya sita ambvazo ni Temeke,Magu,Bukoba Vijijini,Musoma Mjini na Kasulu na wilaya nyingine zikiwa mbiono kuanzisha mtandao huo. 

No comments:

Post a Comment