Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, pamoja na wadau wengine wakati akiwasili nchini Singapore leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Kasulu mjini Mhe Moses Machali pamoja na wadau wengine wakati akiwasili Singapore leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jijini Singapore leo, wakati alipokutana na wafanyabiashara za ujenzi wa nchi hiyo, mara tu baada ya kutua kutoka Japan, alikokuweko kwa ziara nyingine ya kikazi. Katika mkutano huu Rais Kikwete aliwakaribisha wafanyabishara hao, wa Singapore kuja nchini Tanzania kuwekeza katika sekta ya nyumba, wakati wa chakula cha jioni, kilichiandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) nchini humo.
No comments:
Post a Comment