TANGAZO


Thursday, June 6, 2013

Mangwea azikwa kijijini kwao, wengi wajitokeza mazishi yake


Na Kambi Mbwana, Morogoro
MAELFU ya watu walijazana leo katika Mkoa huu wa Morogoro kwa ajili ya mazishi ya msanii Albert Mangwea Ngwair, huku aliyepata naye matatizo nchini Afrika Kusini, Mgaza Pembe M to The P naye akiwa miongoni mwa waliohudhuria mazishi ya Ngwair. (NA HANDENI KWETU BLOG)
 Hapa jeneza la Ngwair linaingizwa karubini, Kijijini kwao Kihonda, ikiwa ni picha inayoonyesha kuwa hatutaweza tena kukutana na msanii huyu hapa chini ya jua. R.I.P Ngwair.....
 Hapa M to The P akilia baada ya kupita kwenye jeneza la Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Kihonda Kanisani jioni yake.
Mama wa Ngwair akizungumza na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Bendera, leo mjini Morogoro, kabla ya mazishi ya msanii huyo wa Hip Hop Tanzania
 Mwili wa Ngwair unaingizwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Inaendelea hapo chini.....


 Mbunge Sugu anamuaga Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Hapa watu wanakanyagana kwa ajili ya kujipanga mstari kwenda kumuaga marehemu Ngwair leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ulikuwa umejaa watu, sambamba na wale waliojipanga barabarani kwa ajili ya kuangalia msafara wa Ngwair uliofunika mji wote siku ya leo.

Tukio la kuzikwa lilitanguliwa na shughuli ya uagaji iliyofanyika pia katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, baada ya kuona mkanyagano wa watu wengi nyumbani, usiku wa Jumatano, ambapo taarifa za kuwasili kwa mwili wa Ngwair zilienea.

Makaburini nako kulikuwa hakutoshi baada ya watu wengi kufurika, huku kila mmoja akiwa na lake, wakiwapo wale waliokwenda kwa ajili ya kuangalia wasanii wao.

No comments:

Post a Comment