Bintiye marehemu Michael Jackson, Paris, mwenye unmri wa miaka 15, amelazwa katika hospitali moja mjini Carlifornia baada ya kujaribu kujiua. Msemaji wa familia ameeleza kuwa anaendelea kupata nafuu na kuwa madaktari wanamshughulikia vilivyo.
Inasemekana, Paris Jackson, ambaye babake alifariki mwaka 2009, amekuwa katika hali ya kusononeka kwa muda sasa.
Msemaji wa familia hiyo amesema kuwa usiku wa kuamkia leo binti huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kujaribu kujiua lakini anaendelea kupata nafuu.
Msemaji alifafanua kuwa hali yake si mbaya sana ya kupelekwa kwa wadi ya wagonjwa mahututi.
Paris Jackson ametajwa kama mmoja wa familia ya Michael Jackson anayetaka kulipwa mamilioni ya Dolar kutoka kampuni ya AEG ambayo ilimwajiri daktari aliyempa madawa Michael ambayo yaligunduliwa baadaye kuwa yalimwua.
Kesi inayohusiana na madai hayo imeendelea kwa majuma sita sasa. Mengi ya kusikitisha juu ya Michael Jackson yamekuwa yakitajwa na inadhaniwa kwamba yamechangia pakubwa kupandisha huzuni na simanzi kwa msichana Paris.
Inadhaniwa kuwa Paris amejaribu kadiri ya uwezo wake kumwomboleza baba yake lakini angali anasononeka kutokuwepo kwake. Mlezi wake kisheria ni nyanya yake Catherine lakini hata hivyo siku chache zilizopita amekuwa akiishi na mamake mzazi.
No comments:
Post a Comment