Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Bi. Ena Mwangama, akimkabidhi kitabu cha sayansi mmoja wa wanafunzi wa shule ya Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa vodacom Tanzania, walipofika shuleni hapo kutoa elimu ya Usalama Barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza Mei 6 hadi 12.kila mwaka.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, wakiwafundisha wanafunzi wa shule ya msingi ya Mapambano ya jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapa msaada wa vitambu vya sayansi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12, ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) kutoa elimu kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini Dares Salaam.
Meneja wa Vodacom Tanzania Grece Lyon (kushoto ) na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Uzuri Tandale ya jijini Dar es Salaam, (kulia)wakionyeshwa vitabu vya sayansi na wanafunzi wa shule hiyo baada ya kukabidhiwa na wafanyakazi wa Vodacom, Ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) kutoa elimu kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini Dares Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Rukia Mtingwa akiwaongoza wanafunzi wa shule ya msingi ya Uzuri iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam, kwenda kujifunza jinsi ya kutumia alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,kila mwaka .Wafanyakazi wa Vodacom waliambatana na Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) Pia walitoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vitabu vya Sayansi.
KAMPUNI ya Mawasiliano
ya Vodacom nchini, leo inaungana na Shirika la Umoja wa Mataifa chini ya Shirika
la Afya Duniani, Makamishna wa Kanda wa Umoja wa Mataifa na Wadau mbalimbali wa
masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya
Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6
hadi 12 kila mwaka duniani kote.
Aidha, katika
maadhimisho hayo, yenye kauli mbiu “Usalama wa Waenda kwa Miguu” na ambayo
yanafanyika kwa msaada wa
Shirikisho la Kimataifa la Mashindano ya mbio za Magari (FIA), lengo hasa ni kutoa elimu kwa watumiaji
wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu juu ya tahadhari wanazopaswa
kuchukua wawapo barabarani.
Akizungumza Dar
es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano Vodacom Tanzania,Bi.Joseline
Kamuhanda, alisema katika maadhimisho hayo wanatarajia kutoa huduma kadhaa
zikiwemo uwezeshaji wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani, na ugawaji wa
zawadi za vitabu kwa wanafunzi wa shule za msingi Tandale Uzuri na Mapambano, jijini
Dar es Salaam.
“Ajali za
barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku
zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila Mtanzania kuwa sehemu ya
kusimamia na kuzingatia sheria za barabarani huku tukijikita zaidi kuchukua tahadhari kwa waenda kwa
miguu kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyotuagiza,” alisema Mwakifulefule na
kuongeza:
Kama Vodacom na
Vodafone duniani kote tumeichagua siku hii kati ya siku saba za mwendelezo wa maadhimisho
haya, ili kujumuika na makundi mbalimbali ndani ya jamii, katika kuelimishana
na kubadilishana mawazo, kwa mantiki ya kila mmoja kuchukua tahadhari, sanjari
na kuzungumza na wanafunzi ambao hasa wengi wao hupata madhara ya kuuawa na
kujeruhiwa kutokana na kugongwa na vyombo vya usafiri wawapo barabarani,”
Aidha, alibainisha
kuwepo kwa ongezeko la vifo vya watembea kwa miguu vinavyotokana na ajali za barabarani kila siku, huku
akisisitiza kuwa ni kadhia inayoleta simanzi na kusababisha kupotea kwa nguvu
kazi ya taifa, sambamba na kuwasihi watanzania kila mmoja kutoa sauti
itakayosaidia kupunguza maafa hayo na ajali nyingine za barabarani kama kauli mbiu
ya mwaka huu inavyotuagiza.
Kamuhanda,
akizungumza kwa niaba ya Vodacom na Vodafone duniani, alisema inapaswa
kueleweka kuwa tafiti zilizopo zinaonesha zaidi ya watembea kwa miguu laki 3,
sawa na robotatu ya watu milioni 1.3 duniani kote hufa na wengine kujeruhiwa
katika barabara mbalimbali duniani kwa mwaka, huku wengine wapatao 5000 ambao
wengi wao ni watoto hufariki kila wiki kutokana na kugongwa na vyombo vya
usafiri duniani.
“Hivyo tunaamini
kwa kutumia njia ya elimu na hamasa juu ya masuala ya usalama barabarani ni
dhahiri itakuwa njia bora na rahisi katika kufikisha ujumbe” alisema Mkuu huyo
wa Kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment