Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na ujumbe wake, wakipata maelezo kuhusu vifaa mbalimbali vya mawasiliano zikiwemo simu katika Ofisi ya Kampuni ya Teknolojia ya mawasiliano ya habari (ZTE), wakati alipotembelea Ofisi za kampuni hiyo leo, akiwa katika ziara ya Kiserikali kwa mwaliko wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, katika Mji wa Nanjing, Jimbo la Jiangsu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na mkewe, Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiwa na Mwenyeji wao, Makamo wa Rais wa Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari (ZTE), Bibi Chen Jie (wa pili kushoto), wakiangalia simu na kupata maelezo ya matumuizi ya simu hizo, walipotembelea sehemu mbalimbali, wakiwa katika ziara ya Kiserikali kwa mwaliko wa kukuza ushirikiano katika nyanja za kiuchumi na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), mkewe Mama Mwanamwema Shein (wa pili) na Balozi Mdogo wa China, anayefanyia kazi zake Zanzibar, Bibi Chen QiMan, wakimsikiliza Dk. Dai Xuelong, wakati alipokuwa akiwaonesha baadhi ya vifaa vya mawasiliano, vilivyotengenezwa na Kampuni ya ZTE, alipotembelea Ofisi za kampuni hiyo, akiwa katika ziara ya Kiserikali nchini China katika Mji wa Najing, Jimbo la Jiangsu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na mkewe, Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakielekea katika chumba maalum cha Mitambo ya Teknolojia ya Mawasiliano katika Ofisi za Kampuni hiyo, Mjini Najing, Jimbo la Jiangsu nchini China, wakiwa katika ziara ya Kiserikali nchini humo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na mkewe, Mama Mwanamwema Shein, wakiwa wamevalia vazi maalum, wakati walipoingia katika chumba cha Mitambo ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari, katika Ofisi za kampuni hiyo, Mjini Najing, Jimbo la Jiangsu nchini China, katika ziara rasmi ya Kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein na mkewe, Mama Mwanamwema Shein, wakiangalia Mitambo ya Teknolojia ya Mawasiliano, ikifanya kazi, walipotembelea katika Chumba Maalum cha Mitambo hiyo, Ofisi za kampuni hiyo, Mjini Najing, Jimbo la Jiangsu nchini China, katika ziara rasmi ya Kiserikali.
Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Elimu za Juu katika Vyuo Vikuu mbalimbali katika Mji wa Nanjing, Jimbo la Jiangsu nchini China, wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Sofitel Luxury Hotel, katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Elimu za Juu katika Vyuo Vikuu vya Mji wa Nanjing, Jimbo la Jiangsu nchini China, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), wakati alipozungumza nao leo, ukumbi wa mikutano wa Sofitel Luxury Hotel, Mjini Nanjing katika jimbo la Jiangsu akiwa katika ziara ya Kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto), akiwa na mkewe, Mama Mwanamwema Shein (kushoto) pamoja na Mawaziri na Maofisa aliofuatana nao katika ziara ya Kiserikali nchini China. Rais alipata muda wa kuzungumza na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Vyuo Vikuu mbalimbali na kuwaelezea hali halisi ya utulivu na amani iliyopo nchini Tanzania na kuwataka kuondokana na wasiwasi.
Mwanafunzi Sauli Elingarama, Daktari wa bianadamu, akiuliza swali mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa mazungumzo na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma, Vyuo Vikuu vya Mji wa Nanjing, nchini China katika Jimbo la Jiangsu. Rais yupo China kwa ziara ya Kiserikali.
No comments:
Post a Comment