TANGAZO


Thursday, May 30, 2013

Balozi wa Eritrea afukuzwa Canada


Canada imewahi kumuonya bwana Micael dhidi ya kuwatoza raia wake kodi
Serikali ya Canada, imemfurusha balozi wa Eritrea nchini humo kufuatia madai kuwa aliwatoza kodi raia wa Eritrea nchini humo ili kufadhili jeshi la nchi hiyo
Semere Ghebremariam Micael, mkuu wa ubalozi wa Eritrea mjini Toronto, amekuwa akichunguzwa kwa madai hayo.
Hatua kama hiyo ya kuchangisha pesa inakiuka vikwazo vya umoja wa mataifa dhidi ya nchi hiyo pamoja na sheria za Canada.
Bwana Micael, amepewa hadi tarehe tano Juni kuondoka nchini humo.
Canada mara kwa mara imekuwa ikiitaka Eritrea kuheshimu sheria za kimataifa na sheria za taifa hilo.''
Kitovu cha Mzozo huo ni juhudi za Eritrea kuwatoza raia wa taifa hilo walio ugenini asilimia mbili ya kodi, kwa ajili ya ulinzi wa taifa lao.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa, lilikaza zaidi vikwazo dhidi ya Eritrea mwezi Disemba mwaka 2011 kuhusu madai ya kuunga mkono wapiganaji wa kiisilamu mfano al-Shabab nchini Somalia. Vikwazo hivyo ni pamoja na kutowatoza raia wake walio ugenini kiwango chochote cha kodi.
Bwana Michael, amewahi kuonywa dhidi ya kuchangisha pesa zozote kutoka kwa raia wa Eritrea walio nchini Canada. Ubalozi hata hivyo umesema kuwa utatii uamuzi wa serikali ya Canda mwezi Septemba.
Lakini hivi karibuni , ripoti zilisema kuwa bwana Michael, alianza tena kuwatoza raia wake kodi.
"Lazima uende kwenye ubalizi kutoa pesa hizo, wanapanga watakavyokutoza pesa hizo,'' raia mmoja wa Eritrea mjini Toronto, alimbia shirika la habari la CBC.
"Wanataka 2%… hawakupi sababu. Lazima utoe pesa hizo,'' alisema mtu huyo.
"Familia yangu inaweza kujikuta kwenye shida ikiwa sitolipa.''
Bwana Michael hata hivyo, amekanusha kuwa alivunja sheria , akisema kuwa yeye alikuwa anatoa taarifa kwa watu waliotaka kutoa mchango wao.

No comments:

Post a Comment